Na Mwamvua Mwinyi, Pwani


SERIKALI Mkoani Pwani, imetoa Rai kwa Taasisi za Serikali zinazohusika na Uwekezaji kuwafikia Wawekezaji pamoja na kutoa Elimu wakati wakiwa kwenye hatua za awali za Uwekezaji .

"Haipendezi kukuta mwekezaji kapewa vibali karibu vyote na kukosa kimoja, Tukae na Wawekezaji tuwaeleweshe waelewe " Amewaeleza Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani,ametoa rai hiyo , wakati alipotembelea Kiwanda cha Futan Mining International Ltd ,kilichopo eneo la Visiga B Kibaha Mjini Kinachojihusisha na kuyeyusha Shaba (Copper Smelting).

Kunenge alifika kiwandani hapo kukagua na kutatua Changamoto ya Wawekezaji hao ,na kusema baadhi ya Taasisi husika za uwekezaji na watendaji zisiwe sehemu ya kukwamisha juhudi za kuinua sekta ya viwanda na uwekezaji.

"Changamoto imejitokeza wamekuja Wawekezaji wamejenga kiwanda kikubwa kimekamilika kwenye eneo la viwanda vidogo ,wamepewa Vibali vyote isipokuwa cheti cha tathimin ya Athari ya Mazingira EIA , hawawezi kuendelea na uzalishaji".

Kunenge ameeleza kuwa Eneo hilo pia ni Eneo la Viwanda Vidogo Lakini bado kuzunguka eneo kuna wananchi wamejenga Makazi jambo ambalo ni kinyume na Mipango miji.

Amemtaka Mkurugenzi wa Mji kusimamia mipango miji "Maamuzi tuliokubaliana eneo hili lipangwe vizuri tuwaeleze wananchi Eneo hili ni Viwanda Vidogo Tutawashirikishe wananchi wasiendelee kufanya maendelezo kwenye eneo hili isipokuwa Viwanda.

Na kwa wale ambao wamepakana na Kiwanda hiki Muwekezaji yupo tayari kutoa Fidia ili aendelee na Uwekezaji" Ameeleza Kunenge.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...