Na Khadija Kalili, Kibiti
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge leo Julai 21 2022 (Jumatano) amesema kuwa Mkoa wa Pwani umejipanga kuandika historia katika kilimo kwa kuanzishwa kilimo cha mazao ya chikichi,alizeti na mazao hayo yalimwa kwa njia ya kisasa ikiwa ni katika kukuza sekta ya kilimo Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.
RC Kunenge amesema kuwa tayari wameshafanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe hivyo Mkoa wa Pwani utaanza kuwa na mashamba darasa na katika sekta ya Kilimo na kuwa utakua Mkoa wa Mfano kwa kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa.
RC Kunenge amesema hayo leo alipokua akizindua na kukabidhi matrekta kumi pamoja na pawatila moja yote yakiwa na thamani ya Mil.700.
Zana hizo za kilimo zilikabidhiwa kwa kikundi cha wakulima wa zao la mpunga ambao pia ni wawekezaji 300 wa ndani kutoka Wilayani Mbarari wanaofahamika kwa jina la Mbakiamtur wamewekeza Wilayani Kibiti tukio ambalo lilifanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi Kibiti, Mkoani Pwani.
Aidha RC Kunenge amewapongeza vijana kutoka Mbarari kwa kuja kuwekeza Mkoani Pwani huku akiwasisitiza vijana wenyeji wa Wilaya ya Kibiti kujifunza na kushirikiana nao kwa ni ni njia mojawapo ya wao kuweza kujiajiri.
Amewataka Viongozi wa Wilaya hiyo kuwasaidia wakazi na vijana kujiunga kwenye vikundi Ili waweze kusaidika kwa njia ya umoja .
Aidha RC Kunenge ametoa shukran kwa Taasisi ya PASS Leasing ambao ndiyo waliotoa mkopo kwa wakulima hao wa zao la mpunga.
Wakati huohuo RC Kunenge amesema kuwa changamoto ya wakulima na wafugaji hasa wafugaji kuvamia mashamba na kulisha mifugo yao analifanyia kazi kwa kuweka mikakati na mipango thabiti na kuwa itabaki kuwa historia ndani ya Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa kikundi wawekezaji Mbakiamtur Hamisi Mohamed Kambaga akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake ametoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Ahmed Abbas Ahmed pamoja Mkuu wa Mkoa kwa kuwapokea na kjwapa nafasi ya kuwekeza Wilayani hapa ikiwa ni pamoja na kuwapa ushirikiano wa kutosha huku akisema kuwa kwa msimu huu watalima ekari 8000 na wanategemea kupata magunia 120,000.
"Tunachangamoto ya miundombinu inayokwenda katika eneo la mradi pia tunaomba Serikali itusaidie vibanio na kutafutiwa eneo la ujenzi wa Kiwanda cha kukoboa Mpunga"alisema.
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema anampongeza Waziri wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe kwa kuleta Mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini kwani hivi sasa kilimo kinameleta tija.
Diwani wa Kata ya Mtunda ambapo ndipo lilipo eneo la mradi huo Mheshimiwa Omari Bakari amesema anashukuru kwa mradi huu mkubwa ambao ni wa kipekee katika kata ya Mtunda huku akikaribusha wawekezaji wengine kujitokeza zaidi.
Matrekta yaliyotolewa kwa mkopo.Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alipokea rusala kutoka kwa Mwenyekiti wa Mbakiamtur Hamisi Mohammed Kambaga.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...