Na Janeth Raphael - Dodoma
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Brazil zimesaini mkataba wa mradi wa utafiti wa mbegu ya pamba,usalama wa chakula na masuala ya lishee wenye thamani jumla ya Dola za Marekani 930,118 kwa lengo la kuimarisa utafiti pamoja na kuongeza Thamani ya zao la pamba hapa nchini.
Wakisaini mkataba huo leo jijini Dodoma akiwepo Balozi wa Brazili Nchini Tanzania,Antonio Cesar,Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP),Gunga Mbavu ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania,Marco Mtunga.
Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP),Gunga Mbavu ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Amesema mradi huo wa BEYOND COTTON PROJECT utanufaisha kaya Zaidi ya kaya 8800 kwa dhumuni la kuimarisha tija katika uzalishaji wa zao la pamba.
“Matarajio yetu wakulima kaya kama 8800 watanufaika katika mradi huu zikiwemo asilimia 50 ya vijana watanufaika na mradi huu utatekelezwa katika mkoa wa mwanza,tumepanga ifikapo mwaka 2030 kilimo kikue kwa asilimia 10,na mradi huu umelenga agenda za kilimo tulizo jiwekea’’ Amesema
Balozi wa Brazili Nchini Tanzania,Antonio Cesan amesema kuwa Brazil wataendelea kushirikiana na nchi ya Tanzania kwa kuimarisha kilimo cha Pamba ili kuwa na tija katika zao hilo.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania,Marco Mtunga ameeleza kuwa pamba ni zao ambalo litaongeza tija kwa mkulima pamoja na vijana kuweza kujikwamua kimaisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mbegu TARI,Dr Geofrey Mkamilo amesema kuwa Taasisi hiyo itaendelea kufanya utafiti wa mbegu bora ambazo zitaongeza tija kwa wakulima wapamba Pamoja na kuleta matokeo chanya kwa wakulima.
Mradi huo wa kilimo cha pamba utatekelezwa katika mkoa wa Mwanza pamoja na wilaya zake ikiwemo Wilaya ya Magu,Misungwi na kwimba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...