Tarehe 14 Mh. Kihenzile akiongozana na mwenyeji wake Mbunge wa jimbo la Monduli Mh. Fredrick Lowassa amepokea ugeni wa Tanzania Red Cross Society ukiongozwa na rais wa wao ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile katika Kijiji cha Donyonadoo ikiwa ni mojawapo ya vijiji vilivyoathiriwa na ukame kwa kiasi kikubwa na hivyo shirika la TRCS limetoa msaada wa kiasi cha Shilingi 210,000 katika kaya 114 zilizopelekea jumla ya shilingi Milioni 23 kugawiwa kwa wanakijiji hawa ili kusaidia kujikimu na kupunguza makali ya athari wa ukame huo. Akizungumza na wananchi hao
Akizungumza Rais wa Shirika hilo (TRCS) Mh. David Mwakiposa Kihenzile Ambaye Ndiye Mgeni rasmi katika zoezi la Ugawaji wa Fedha hizo amesema wamejikita hasa kutoa Misaada ya kibinadamu kabla na baada ya Maafa , Ambapo Msaada huo unalenga Kaya zilizoathirika na Maafa ya Mifugo Mwaka jana .
Kihenzile ameongeza kuwa Wanagusa Familia zilizoathirika na Ukame, Ambapo jumla ya vifo vya Mifugo ni Punda zaidi ya elfu 2 Ng’ombe zaidi ya elfu 41,Mbuzi zaid elfu 34, na Kondoo zaidi ya elfu 54, kwa Wilaya ya Monduli, na kusema pamoja na kutoa Fedha taslim pia wametoa vyombo vya kuhifadhia maji ya nymbani,dawa za kutibu maji (vidonge),chakula lishe kwa watoto wenye utapiamulo,elimu ya kupinga ukatili na umuhimu wa shule kwa mtoto wa kike. Hivyo basi Jumla ya Fedha zilizotolewa kwa Mikoa ya Manyara na Arusha ni Jumla ya Millioni 216 kwa kaya elfu Moja na Mia mbili (1200).
Mh. Kihenzile amewataka wananchi wa donyonadoo kuwa wanachama na voluntia wa TRCS kwani yapo mambo ambayo watanufaika nayo kwakusaidiana wao kwa wao ikiwemo mafunzo ya huduma ya kwanza na wasiishie kuitambua TRCS kam chombo cha kuwasiaida waathirika na wahanga tu bali watambue yakuwa Red Cross popote Dunainai inajengwa na watu wanaojitolea kwaajili ya watu wengine kwani hata msaada huo walioupata wapo watu kutoka nchi mbali mbali kupitia IFRC wamejitolea kwaajili yao ili kuwapunguzia maumivu kwa madhira walioyoyapata.
Fredrick Lowassa ni Mbunge wa jimbo la Monduli ambaye ndiye mwenyeji Katika ziara ziara hiyo Amemshukuru Rais wa TRCS kwa Kufika idonyonaado, na Kusema mchakato huo ni wa kitaalamu , Miundombinu ya idonyonaado ni changamoto kupatikana kwa maendeleo Hivyo anawashukuru sana TRCS chini ya uongozi wa Mh.Kihenzile kwakuweza kuwafikia wananchi hao ambao sio rahis kila mtu kuwafikia nakuomba TRCS iendelee kuwa karibu nao kwani wamesitiriwa kiasi kwamba wote wanaridhia kuwa mabalozi wazuri wa Red Cross. Vilevile Mh.Fredrick Lowassa amekiri kutambua mchango mkubwa walioutoa nakuwaomba wasiiishie hapo kwani TRCS ni kisaidizi cha serikali kama ambavyo inajulikana hivyo basi waendelee kuwa bega kwa began a serikali ya awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassani kuhakikisha jamii zote zipo salama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...