Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussen Bashe, amewataka wadau wa tasnia ya sukari kuwa na imani pamoja na kujenga mahusiano mazuri na Bodi ya Sukari ili kuimarisha zao la miwa na kukuza soko la sukari nchini.

Waziri Bashe ameyasema hayo leo mchana Julai 15, 2022, kwenye ukumbi wa hotel ya Morogoro wakati akizindua Kongamano la 10 la Wadau wa Sukari ambapo lilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.

Waziri Bashe amesema Serikali ya Awamu ya Sita imesikia hofu waliyonayo wadau sukari juu ya sera na kuwahakikishia kuwa Serikali italinda uwekezaji wao wanaofanya nchini pamoja na kuwaunga mkono katika juhudi zao za uzalishaji wa sukari.

Aidha, Waziri Bashe ameiagiza Bodi ya Sukari pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) kuanzisha mashamba ya kuzalisha mbegu bora ili kuongeza tija na uzalishaji zaidi wa miwa nchini.

“Tuna aina mbili za mbegu ya zao la miwa; Ni lazima tukubaliane kuanzisha mashamba yatakayozalisha mbegu”. Amesisitiza Waziri Bashe.

Waziri Bashe pia ameagiza kufanyiwa maboresho kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Sukari ili uweze kutatua changamoto mbalimbali na kuendeleza tasnia hiyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...