*Utaratibu huo umeanza Julai 20 kwa kampuni iliyopewa zabuni hiyo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHRIKA la Viwango Tanzania ( TBS) limesema kuwa metoa kuanzia Julai 20, 2022 magari yote yaliyotumika yanayotoka nchini Japan yatakuwa yanakaguliwa nchini huko na kila gari litakaguliwa kwa dola za kimarekani 150 kabla ya kuja Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi wa TBS Mhandisi Said Issa Mkwawa amesema kuwa ukaguzi magari hayo utafanywa Nchini na Kampuni ya EAA Company Limited ya nchini Japan.

Amesema kuwa taratibu za kuipata kampuni hiyo zimetumika kwa mujibu wa sheria za nchi na vigezo vilivyokuwa vimeanishwa vimefuatwa na kampuni hiyo.

Mhandisi Mkwawa ameongeza kuwa utaratibu huo utasaidia kuepuka gharama za matengenezo kwa wanunuaji wa magari ambacho kilikuwa kilio cha wadau wetu wa waagizaji na wauzaji wa magari

Amesema katika ziara za Rais Samia Suluhu Hassan hiyo kwa TBS ni mafanikio ya kufungua mipaka ya kibiashara na katika kurahishisha kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo magari yanayotoka nje ya nchi.

Amesema Shirika linaendelea na taratibu za kupata mawakala kwa ajili ya ukaguzi wa magari yanayotoka Nchi za Uingereza, Dubai na Singapore na utaratibu huo utakapokamilika basi waingizaji na wafanyabiashara wa magari watapewa taarifa.

Aidha kwa magari yaliyoko njiani na meli yatakaguliwa yakifika nchini kwani zoezi hilo kwa tararibu za kampuni ya ukaguzi umeanza Julai 20 mwaka huu.
Meneja wa Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Mhandisi Said Issa Mkwawa akizungumza na waandishi habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...