Na Mwandishi Wetu
HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam imeanza ujenzi wa mradi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu, Netboli na basketball kwenye eneo la wazi la Mwembeyanga ndani ya Manispaa hiyo pamoja na kuboresha maeneo mbalimbali kwenye eneo hilo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo ameeleza kwamba ujenzi wa maeneo hayo ya wazi ndani ya Wilaya hiyo likiwemo la Mwembeyanga unatarajia kugharimu Sh.milioni 998 mpaka utakapokamilika.
Amesema mradi huo utausisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu kwa kupanda nyasi na kujenga miundombinu yake, na kufanya kuwa wa kisasa."Mradi huu ukikamilika utalifanya eneo hili maarufu la Mwembeyanga ambalo limesheheni historia ya nchi yetu kuwa la kisasa zaidi kwa kuwa na miundombinu rafiki.
"Naufahamu hapa pamekuwa pakitumika kwa michezo mbalimbali, matamasha na mikutano, kukamilika kwake kutapafanya wananchi wa maeneo haya kuwa na sehemu sahihi ya kufanya michezo na kupumzika," amesema Jokate
Ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi ambao umefikia asilimia 25 kwa sasa wananchi wataendelea kupatumia bure kwa shughuli za michezo na za kijamii inavyotumika na hakutakuwa na gharama yoyote.
Amesisitiza kuwa eneo hilo litakuwa chini ya Halmashauri lakini Wananchi wataendelea kushirikiana nao katika kutekeleza masuala mbalimbali na hakuna gharama yoyote katika kulitumia eneo hilo.
Jokate amesema mbali ya kuboresha maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya ya Temeke kupitia Mradi huo wa kulipendezesha jiiji la Dar es Salaam ikiwemo Wilaya hiyo wanatarajia kupanda miti ya aina mbalimbali zaidi ya 1900.
Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo kutoka Wakala wa ujenzi wa baraara mjini vijijini (TARURA) Manispaa ya Temeke Mhandisi Paul Mhere amefafanua mkataba wa mradi huo na kampuni ya ujenzi ya Group Six International utakamilika ndani ya miezi miwili,hivyo Agosti mwaka huu mradi utakuwa umekamilika.
"Kazi kubwa kwenye Uwanja wa mpira wa miguu Kwa mfano, ilikuwa kuweka levo uwanja na kuupima katika vipimo vinavyokubalika kama viwanja vingine rasmi vya mpira, baada ya hapo ni kuotesha nyasi za kisasa na kujenga miundo mbinu yake kuzunguma uwanja.Kazi imeshaanza mpaka sasa ndani ya wiki mbili tumeshafikia asilimia 25 ya ujenzi, "amesema.
Home
HABARI
TEMEKE WAANZA UBORESHAJI MIUNDOMBINU MAENEO YA WAZI, MWEMBEYANGA KUJENGWA VIWANJA VYA MICHEZO VYA KISASA...JOKATE ATOA NENO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...