Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KLABU ya Yanga inamuunga mkono, Msemaji wake, Haji Manara kwa kudai haki kwenye vyombo vya juu vya Kimataifa baada ya Msemaji huyo kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili na faini ya Shilingi Milioni 20 na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo imeeleza kuwa Yanga inaamini Haji Manara hakutendewa haki kwa adhabu hiyo aliyopewa na Kamati hiyo ya Maadili ya TFF.

“Adhabu hii inakwenda kuathiri moja kwa moja mchango wa Ndugu Haji Manara katika maendeleo ya mpira wa miguu kwenye Klabu yake ya Yanga, Ligi Kuu ya Zanzibar, Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pamoja na nchi jirani (Burundi) ambazo amezihudumu katika nyadhifa mbalimbali za uhamasishaji na ukuaji wa mpira wa miguu”, imeeleza Yanga SC kupitia taarifa yake

Hata hivyo, Yanga SC kupitia taarifa hiyo imeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Kamati ya Maadili ya TFF dhidi ya Msemaji wao, Haji Manara.

Kamati ya Maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Mwita Waissaka na Katibu wake, Walter Lungu imetoa hukumu dhidi ya Haji Manara baada ya  kukutwa na makosa ya kumtishia, kumdhalilisha Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) kati ya Yanga ScC dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijinri Arusha, Julai 2, 2022.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...