Mdau wa Maendeleo, Benedict Amandusi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo Julai 7, 2022.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano TIC, Pendo Gondwe akizungumza na Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo Julai 7, 2022
MWANANCHI na Mdau wa Maendeleo, Benedict Amandusi amewashauri Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kutoa elimu kwa wananchi ili kila mtu anufaike na fursa zilizopo Nchini.
Ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo Julai 7, 2022. Amesema kuwa wananchi waelimishwe pia wajue namna ya kuangalia tovuti ya Kituo hizo ili kujua fursa zilizopo za uwekezaji na biashara.
Amandusi amesema kuwa TIC lazima iangalie namna ya kutoa elimu kwa wananchi wote kwa sababu sio Watanzania wote wanaweza kujifunza kwa kutumia tovuti.
Pia amewapongea TIC Kushiriki katika maonesho hayo kwa sababu wanatoa elimu kwa kila anayetembelea banda lao na kuunganisha taarifa za taasisi mbalimbali zinaazohusiana na Biashara na Uwekezaji kwa wawekezaji.
Taasisi zilizounganishwa katika Mfumo wa Mtandao Mmoja ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania( TIC), taasisi inayohusika na Vibali vya kufanya kazi (Work Permity), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Wizara ya Ardhi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA).
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Taasisi nyingine ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Uhamiaji.
Amesema kwa Upande wake amenufaika kwa kutembelea Banda la Viwanda na Biashara kwani limesheheni taasisi mbalimbali.
"Nimeona kituo cha Uwekezaji katika Tovuti lakini nikaona haitoshi nimekuja katika banda hii kufuatilia na kuona ni Fursa gani zilizopo hapa nchini katika Biashara." Amesema Amandusi
Amesema kuwa amenufaika na huduma zinazotolewa kwani kila taasisi inayohusika na Uwekezaji ipo katika banda hili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...