
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbrt Kabyemela aliyeshia simu akizungumza na mteja ambaye aliibuka mshindi katika shindano la Mchezo wa Kubahatisha la TRA ambapo Mteja amenunua bidhaa na Kudai Risiti halali katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
WASHINDI wanne wa shindano la Kubahatisha linaloendeshwa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta wamejishindia kila mmoja kiasi cha shilingi laki Mbili na elfu Hamsini Jijini Dar Es Salaam leo Julai 18, 2022.
Akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kuwapata washindi hao,
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka hiyo, Herbert Kabyemela amesema kuwa Mchezo huo wa kubahatisha unaosimamiwa na bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini kila mwananchi anayenunua bidhaa na kudai risiti atakuwa ameingia moja kwa moja katika droo ya kujishindia fedha kila Juma tatu ya mwezi wa Julai hadi Septemba.
Amesema kuwa kila mwezi kutakuwa na droo kubwa ambapo mshindi atapata kiasi cha Shilingi Milioni Moja na kila Juma tatu washindi wanne wa laki mbili na elfu hamsini watatangazwa.
"Na leo ndio Juma tatu ya kwanza ndio tumeanza na tumepata washindi wanne ambao wamejishindia kiasi cha laki mbili na Elfu hamsini kila mmoja, hii ni kwa wale tuu walio nunua bidhaa na kudai risiti halali yenye namba yao ya simu." Amesema Kabyemela
Amesema kuwa lengo la kuwa na Mchezo huo katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta ni kuhamasisha wakazi wa maeneo hayo wanunuapo bidhaa mbalimbali wadai risiti halali.
Amewakumbusha wananchi wanaonunua bidhaa kudai risiti na wanaouza bidhaa mbalimbali watoe risiti ili waingie katika droo ya kujipatia zawadi kutoka TRA.
"Tunategemea wananchi watadai risiti kwa wingi wanapofanya manunuzi ili waweze kushiriki droo hii, kwa namna hiyo risiti zitatolewa na kuweza kuboresha mapato ya sirikali." Amesema Kabyemela
Amesema kuwa Mwananchi anayetoka maeneo ya mikoa ya kikodi mingine anaweza kwenda kununua bidhaa katika mkoa wa kikodi wa Tegeta na kudai risiti na anaweza kuingia katika droo ya mchezo huo wa kubahatisha na baadae kunishindia zawadi kutoka TRA.
"Hatuangalii munuaji ametoka wapi bali tunaangali amenunua bidhaa kutoka Mkoa wa Kikodi wa Tegeta tuu." Amemalizia Kabyemela
Aidha ametoa rai kwa wananchi kununua bidhaa katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta na kudai risiti kwa wingi ili wawe na Kumbukumbu ya bidhaa walizonazo na kumbukumbu hizo ziwe kwenye mifumo ya TRA.
Kwa Upande wa Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Tegeta, Mazula Mtwale ameyataja maeneo ambayo mwananchi anatakiwa kununua bidhaa na kudai risiti halali ili uingie katika shindano hili ni Tegeta, Goba, Mbezi Beach, Bahari Beach, Ununio, Mabwepande, Boko, Madale, Wazo, Mbopo, Salasala, Kunduchi na Bunju.
"Hakikisha unapata risiti iliyohalali iliyoandikwa namba zako za simu ili uweze kuingia katika droo ya kipekee na utashinda shilingi 250,000 (Laki Mbili na Elfu hamsini) kwa washindi wanne wa kila wiki, tukumbuke mwisho wa Mwezi tutakuwa na Bahati nasibu kubwa kabisa na itakuwa na mshindi wa mwezi ambaye atapata shilingi milioni Moja (1,000,0000) lakini washindi wa Kila Juma tatu watakuwepo." Amesema Mtwale
Hata hivyo amewakumbusha Mwananchi wanaponunua bidhaa wadai risiti iliyohalali ili kuweza kuingia katika droo ya Kipekee na kujishindia pesa kutoka TRA.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbrt Kabyemela akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam wakati wa Kuwatangaza washindi wa shindano la kununua bidhaa na kudai Risiti halili katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano la Mchezo wa Kubahatisha la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam kwa kununua bidhaa na Kudai Risiti halali yenye namba ya simu ya Mteja.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbrt Kabyemela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa Kuwatangaza washindi wa shindano la kununua bidhaa na kudai Risiti halili katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...