Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania umeelezwa kufurahishwa kwake na mafanikio makubwa yalioanza kuonekana katika utekelezaji mradi wa kuinua ushiriki wa wanawake katika uongozi Zanzibar (SWIL)

Mradi huo unaotekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Asasi nyengine za kiraia ikiwemo ZAFELA na PEGAO na hadi sasa umefikia wananchi wapatao 6917 Unguja na Pemba huku wanawake wakiwa ni 4797 na wanaume 2120.

Wakijadili utekelezaji mradi huo katika ofisi za TAMWA-ZNZ zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja maafisa hao wakiongozwa na Bjorn Midthum walisema kuna mengi makubwa yameonekana kwenye mradi huo kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuanza kwake mwaka 2020 hadi sasa.

Alisema kuna idadi kubwa ya wanawake wengi zaidi waliojitokeza kugombea na kushinda nafasi tofauti za uongozi kuanzia kwenye vyama vya siasa na asasi za kiraia.

Alieleza kuwa mabadiliko hayo yote anaamini yamekuja kutiokana na nguvu kubwa kupitia mradi huo na hatimae kwa mara ya kwanza wanawake wengi zaidi wamehamaisha na kujitokeza kugombe amaa kupaza sauti zao.

Pia alisema kupitia vijana maalumu ambao wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanajamii (CBS) wamefanya kazi kubwa ya kuhamaisha jamii sambamba na kuongeza kasi ya uwajibikaji kwa viongozi na kasha viongozi hao kuwajibika katika jamii ikiwemo kuwasaida wananchi wao katika changamoto zinazowakabili kwa baadhi ya maeneo.

Alisema awali wakati mradi huo unaanza kulikua na changamoto nyingi za wanawake visiwani hapa ikiwemo baadhi ya wanawake wengi kushindwa kufahamu kama wao ni sehemu ya jamii na wanapaswa pia kuwa viongozi bali wengi wao waliamini anaepaswa kuwa kiongoni ni mwanamme pekee.

Alisema kwa sasa changamoto hio imeanza kuondoka kwa kasi kubwa na ndio maana kuna idadi kubwa ya wanawake wanaendelea kujitiokeza katika kila chaguzi ziwe za kitaifa au za kichama.

Aidha afia huyo alisema mafanikio yote yaliopatikana kwa miaka miwili ya utekelezaji mradi yamekuja kutokana pia na nguvu kubwa ya vyombo vya habari ambavyo vinasaidia kupaza sauti za wananchi waliokosa sehemu ya kupaza sauti hiozo kwa muda mrefu.

‘’Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wanahabari wote wanaoendelea kushiriki na kufanya kazi kwenye mradi huu kwa hakika wamefanya kazi kubwa sana inayopaswa kupongezwa na kila mmoja’’aliongezea.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alishukuru mashirikiano na Ubalozi Norway Tanzania katika utekelezaji mradi huo na kuahidi kuendelea kuwafikia wengi zaidi ili kuleta tija.

Alisema mafanikio hayo ya awali yamekuja kutokana na ushirikiano wa karibu kutoka katika Ubalozi huo na anaamini kuwa mafanikio makubwa zaidi yatapatikana na hatimae Zanzibar iweze kuingia kwenye historia ya kuwa na idadi kubwa ya viongozi wanawake.


Meneja miradi TAMWA-ZNZ Alli Mohamed akiagana na Afisa Ubalozi wa Norway Tanzania Bjorn Midthum mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliolenga kutazama utekelezaji radi wa SWIL.
.Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...