WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb), amemteua Bw. Imani Joel Kajula kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT) kwa kipindi cha miaka mitatu. Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5 (4) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245 kikisomwa kwa pamoja na Aya ya 2.2 ya Amri ya kuanzishwa kwa Chuo hicho cha Taifa cha Utalii. Aidha, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT): -


  1. Prof. Wineaster Anderson, Prof. Mshiriki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Shule ya Biashara;

  2. Bw. Matendo Bwire Manono, Wakili Mkuu II, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

  3. CPA. Suzana Steve Chaula, Mhasibu Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE);

  4. Bw. Enock Robert Wagala, Mkurugenzi wa Mipango, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA);

  5. Bibi Gerwalda Florence Luoga, Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).


Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Julai, 2022 hadi 11 Julai, 2025.


Imetolewa na;

Aron Msigwa

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...