Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde, amesema zoezi la usajili wa wakulima nchini linaloendelea litasaidia kurahisisha utoaji wa huduma za msingi kwa wakulima na pia litazuia udanganyifu uliokuwa ukijitokeza kwa baadhi ya watu kunufaika kwa mgongo wa wakulima
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Julai 6, 2022 alipotembelea na kukagua Ujenzi wa Ghala kwa ajili ya kudhibiti tatizo la Sumu kuvu unaotekelezwa na Mradi wa TANIPAC katika Kijiji cha Mrijo chini, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Ujenzi wa Ghala hilo ni moja kati ya Maghala 14 ambayo yanajengwa maeneo mbalimbali nchini ambapo ujenzi wake umegharimu kiasi cha Bilioni 14 huku gharama za ujenzi wa ghala hilo la Kijiji cha Mrijo chini kikiwa Shilingi Bilioni 1.04.
“Nafikiri wote ninyi ni mashahidi na mliona Waziri Bashe akizindua zoezi la usajili wa wakulima ambalo lengo lake ni kuwatambua wakulima na kuweza kuwahudumia kirahisi hasa katika eneo la pembejeo.
Kumekuwepo na watu wachache ambao sio waaminifu ambao wamekuwa wakinufaika kwa mgongo wa wakulima,kupitia usajili huu tunakwenda kuzuia watu kunufaika kwa udanganyifu kwakuwa tutwakuwa na uwezo wa kuwatambua wakulima wetu.
Leo nipo hapa kukagua ghala hili kubwa linalojengwa chini ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan,ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti sumukuvu.
Niwaombe muutunze mradi huu na muulinde ili tuweze kufikia matarajio na malengo tuliyojiwekea”Alisema Mavunde
Akitoa maelezo ya awali,Mratibu wa Mradi wa TANIPAC Ndg. Clepin Josephat amesema sambamba na ujenzi wa maghala unaofanyika hapa nchini pia mradi huu utahusisha utoaji wa elimu kwa wakulima juu ya uhifadhi wa mazao baada ya mavuno ikiwa ni mkakati wa awali wa kudhibiti sumukuvu.
Nao Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mh. Simon Chacha na Mbunge wa Jimbo la Chemba Mh.Mohamed Moni wameishukuru serikali kwa utekelezaji wa mradi wa kudhibiti sumukuvu kwa kujenga ghala kubwa kijijini Mrijo ambalo litasaidia katika uhifadhi wa mazao ya wakulima baada ya mazao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...