Mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam, Omary Kumbilamoto akionyesha simu aina ya smart kitochi aliyonunua kwenye banda la Vodacom, Katikati ni Mkurugenzi wa kitengo cha Dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamando na Meneja wa maduka ya rejareja Vodacom, Vanessa Mlawi
Mshindi wa gari kupitia shindano la Vodacom Tusua mapene, Abdulrazak Selemani mkazi wa Mbagala akiwa ndani ya gari mpya aina ya Suzuki S Presso alilojishindia katika shindano la Tusua Mapene lililochezeshwa kwenye maonesho ya 46 ya Biashara ya kimataifa (Sabasaba). Wengine ni Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam, Omary Kumbilamoto (katikati) na Mkurugenzi wa kitengo cha Dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamando.
Mshindi wa gari kupitia shindano la Vodacom Tusua mapene, Abdulrazak Selemani mkazi wa Mbagala akionyesha funguo ya gari mpya aina ya Suzuki S Presso alilojishindia katika shindano la Tusua Mapene lililochezeshwa kwenye maonesho ya 46 ya Biashara ya kimataifa (Sabasaba). Wengine ni Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam, Omary Kumbilamoto (katikati) na Mkurugenzi wa kitengo cha Dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamando. Ili kujishindia zawadi katika shindano hilo tuma neno V kwenda 15544.
KAMPUNI ya Mtandao wa simu za Mkononi Vodacom imepongezwa kwa kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto kwenye jamii
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 7 2022 na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya sabasaba alipokuwa akimkabidhi mshindi wa Shindano la ‘Tusua Mapene’ aliyeshinda gari na kuzitaka Kampuni nyingine kuiga mwenendo wa Vodacom.
Kumbilamoto amesema Vodacom imekuwa sehemu ya kuisadia Serikali kupitia huduma mbalimbali zitakazotoa suluhisho ya matatizo kwenye jamii.
‘’Huyu tayari amepata mtaji na itakuwa sehemu ya ajira kwake gari hii itakwenda kumsaidia kujiingizia kipato “.
Pia ametaja mfano wa changamoto ambayo Vodacom imeitatua ni kurahisisha huduma za kiafya kwa wajawazito.
“Nimefurahi sana mmesaidia kina mama wajawazito kwa kuwarahisishia kuzifikia huduma za Afya mmekuwa mkiiunga mkono serikali kwa vitendo”amesema Kumbilamoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kitengo cha Dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamando amesisitiza kuwa mtandao huo mbali na kuwa na shindano linalowanufaisha Watanzania wanaoshiriki kwenye “Tusua Mapene’ na kupatiwa gari mpya aina ya Suzuki ...pia imejikita kwenye kuwasogeza wakulima karibu na soko kwa kuwarahishishia njia ya Malipo kupitia M Pesa. Tunashuhudia Komondo amesema kuwa Vodacom inaishukuru serikali kwa kuzifanya huduma za kuolewa kuwa rahisi kwa kupuza Tozo.
“Tunaishukuru serikali kwa kupunguza tozo na hivyo tu naendelea na kuhamasisha Matumizi ya Mpesa”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...