Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKUU wa Idara ya uchunguzi wa ARIPO Kanda ya Afrika na Mtaalam wa Uhakiki miliki bunifu(Hataza) Flora Mpanju ametoa ushauri kwa wabunifu wote nchini Tanzania kuhakikisha baada ya kufanya ugunduzi ni vema wakazisajili Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA).

Amesema lengo la kuweka bunifu hizo katika usajili ni kuhakikisha zinakuwa salama ili asitokee mtu mwingine akaichukua na kisha kukimbilia kuisajilli na kumfanya aliyegundua kuibiwa ubunifu wake.

Akizungumza katika banda la BRELA katika ya Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Mpanju amesema yeye ni Mtaalam wa kuhakiki miliki bunifu zinazoletwa barani Afrika kwa ajili ya kuja kupata ulinzi kwenye nchi 21 za za bara hili ambapo makao makuu yako Harare na Tanzania ikiwa ni mwanachama mmoja wapo.

"Nimekuja kwa mualiko wa BRELA lengo la kuja kuwasaidia kuangalia ubunifu unaoneshwa hapa kwenye maonesho na tuwasaidie kutoa maoni yetu. Kwa kweli tumezunguka katika vyuo vyote, tumezungukia watu chungu mzima.

“Nilichokiona ubunifu uliopo hapa Tanzania ni mkubwa mno kiasi kwamba sikutegemea na ni teknolojia ya kisasa.Ubunifu huu tukiuacha bila kuulinda itakuwa ni hasara kwa taifa na Afrika,”amesema.

Amefafanua amewauliza wabunifu hao kama wameshiandikisha bunifu zao BRELA lakini wengi wamekuwa wakishangaa na wala hawajui kama wanatakiwa kusajili.

“Sasa nikawa nawauliza je mimi nikikusiliza kuhusu ubunifu wako halafu nikaenda kusajili BRELA utafanye? Hawana majibu , kwa hiyo ninaiomba Serikali iangalie hili jambo kama ni jambo kubwa,"amesema.

Amesema ni vema wabunifu wakasajili BRELA kama sehemu ya kuweka ulinzi na kujilinda ili asitokee mtu wa kuiba kazi kubwa na nzuri inayofanywa na wagunduzi.

“Kwa mfano tuko kwenye haya maonesho inaruhusiwa miezi mitatu uwe umeshaandikisha na BRELA kama usipoandikisha ina maana ikienda kuhakikiwa itakuwa sio mpya kwasababu ulieleza wewe mwenyewe.

"Kwa hiyo tunaowamba wabunifu kabla hamjenda kwa watu kupiga kelele kuhusu bunifu zenu kuwaambia mimi mmegundua kwanza nendeni BRELA mkasajili ili kupata ulinzi,"amesisitiza.

Aidha amesema iko haja ya kuwepo kwa sera itakayosaidia wabunifu tangu wanapokua shuleni na vyuoni zile gunduzi zao zinakuwa zinalindwa kwa mujibu sera zitakazokuwepo.Pia ameshauri kuwepo kwa mfuko wa fedha ambazo zitasaidia kuwawezesha wagunduzi kusajili bunifu zao.

"Tunaomba Serikali kuangalia katika hilo, nimefurahi kuona ugunduzi unaoendelea Tanzania na sikuamini , nimezunguka nchi nyingi duniani lakini hii niliyoiona hapa ni ya kipekee kwa hiyo nawapongeza na muendelee na maonesho kama hayo.”

Kuhusu muako wa wagunduzi kusajili bunifu zao, amesema muamko haukuwepo kwasababu hakukua na uelewa wa jambo hilo."Wengi wamenisikiliza na kila mmoja anashangaa.”

Ametumia nafasi hiyo kuwapongeza BRELA kwa kazi nzuri wanayoifanya nchini Tanznaia ya kuendelea kuhamasisha watu kujisajili katika wakala huo.


Mkuu wa Idara ya uchunguzi wa ARIPO Kanda ya Afrika ambaye pia ni Mtaalam wa Uhakiki miliki bunifu(Hataza) Flora Mpanju akifafanua jambo alipokuwa katika banda la BRELA.Ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wabunifu kuhakikisha wanasajili bunifu zao ili ziwe salama.

Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA) wakiendelea kuwahudumia wananchi waliofika kwenye banda la Wakala huo lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Mmoja ya maofisa wa BRELA akiendelea kutoa huduma kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la Wakala huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...