Na Karama Kenyunko Michuzi TV

WAFANYABIASHARA sita wakazi wa Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya ukwepaji kodi na kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya Sh bilioni 8.6.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya ukwepaji kodi, matumizi yasiyo sahihi ya mashine za kielektroniki (EFDs) na kusababisha hasara.

Katika hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani hapo na  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Emmanuel Medalakini imewataja washitakiwa hao kuwa ni, Ibrahim Magenge (32) Mkazi wa Kijichi, Eliyasau Mohamed (29) Mkazi wa Buza,
Elisha Numvile (29) Mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ali, Juma Samatta (47) Mkazi wa Kigogo na Siraji Mtungule (32) Mkazi wa Makongo Juu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo imedaiwa kuwa kati ya Januari  na Juni 29, 2022 huko katika maeneo ya Kariakoo, Ilala jijjni Dar es Salaam washitakiwa kwa pamoja walitoa risiti ya uongo kwa kwa kutumia mashine ya kielektroniki ya EFD iliyosajiliwa kwa jina la  Bupe Millinga  yenye namba ya mlipakodi  TIN 135-563-382.

Imedaiwa, mashine hiyo ilikuwa na taarifa za mauzo ya Sh bilioni 17.8 na kusababisha ukwepaji kodi ya ongezeko la thamani ya Sh bilioni 5.3.

Katika shitaka la pili, imedaiwa washitakiwa hao kwa pamoja walikwepa kodi ya ongezeko la thamani ya Sh bilioni 3.3 kwa kutumia mashine hiyo.

Katika shtaka la tatu na la nne, Medalakini amedai katika tarehe hizo washtakiwa walitumia mashine ya EFDs kukwepa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Sh bilioni 8.6.

Amedai kuwa kati ya Januari na Juni 29,2022 maeneo ya Kariakoo Dar es Salaam, washitakiwa walitumia mashine isiyo sahihi ya Milinga  kuonyesha ina mauzo ya zaidi ya Sh bilioni 17.8 kwa lengo la kumdanganya Kamishna wa Mkuu wa TRA na kukwepa kodi ya Sh bilioni 3.3.

Pia washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia TRA hasara ya Sh 8,691,535,718.50.

Kwa mujibu wa upande  wa mashtaka upelelezi katika  kesi kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 21,2022.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu. washitakiwa wote wamerudishwa rumande.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...