Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,kimetoa onyo kwa wanachama wanaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuacha chuki ,kuchafuana na kusigana ,kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani ya Chama kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka miongozo ya uchaguzi.

Aidha zaidi ya wanachama 50,000 wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Jumuiya na chama katika mkoa huo.

Akielezea ,hali ya uchaguzi unaoendelea Kaimu Katibu wa Chama mkoa wa Pwani ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoani humo Elisante Msuya alisema , wanafuatilia muenendo na kusimamia mfumo wa uchaguzi huo kwa kufuata miongozo na kanuni na kusisitiza atakaebainika atakatwa jina kwa mujibu wa taratibu.

Alieleza , Kuna baadhi ya wagombea ambao wameanza kusigana Jambo ambalo halikubariki.

"Haijapata kutokea wanachama kujitokeza kwa wingi namna hii kuanzia ngazi ya tawi ,maana unakuta nafasi moja inagombewa na watu 20 " alifafanua Msuya.

"Tatizo tu tunapata wakati mgumu katika mchujo kwani tunapaswa kufuata kanuni kupitia vikao husika ili kupata watu makini " 

Vilevile, Msuya alibainisha kwamba wameshamaliza chaguzi ngazi ya matawi na sasa wapo wanafanya uchaguzi wa Jumuiya kata ambapo wamefikia asilimia 95  katika kata 133 licha ya kujitokeza dosari kidogo kwenye kata sita ambazo zimebakia kutomaliza uchaguzi kutokana na maelekezo waliyopewa kurudia chaguzi .

Alipoulizwa kuhusiana na tetesi za baadhi ya viongozi na watendaji wa CCM kuhusishwa kwenye uuzaji wa eneo katika Ranch ya RAZABA Bagamoyo linalomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Msuya alikana kwamba ,mkoa hauna taarifa hizo na haijawahi kusikia Kama yupo kiongozi aliyehusika na matukio hayo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...