Muongoza watalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Chalse Karoli, akiwafanunulia jambo, wanafunzi wa Chuo cha Sukari cha Taifa (NSI) kilichopo Kilombero, Mkoani Morogoro,  wakati walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. 
 

WANAFUNZI wa Chuo cha Sukari cha Taifa (NSI), kilichopo Kilombero, Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, kwa lengo la kuunga mkono jitahida za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu, Mkuu wa Chuo cha Sukari Cha Taifa, Aloyce Kasmir, alisema kuwa uongozi na wanafunzi wa chuo hicho wanaosoma kozi ya Teknolojia ya uzalishaji wa miwa na sukari wameamua kutembelea hifadhi ya Mikumi  kwa lengo la  kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika  kuhamasisha watanzania na wageni wa mataifa mengine duniani kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini, sambamba na kuwapa fusra wanafunzi wa chuo hicho  cha Sukari cha Taifa kutambua vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Akizungumza na wakufunzi na wanafunzi wa chuo hicho, Mhifadhi  Daraja Kwanza, Mkuu wa kitengo cha Utalii, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Herman Baltazari, aliwaasa wanafunzi wa ngazi mbali mbali za elimu  kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, kwa kuwa kufanya hivyo kunawapa fursa ya kutambua uzuri wa nchi, rasilimali zilizopo  na kuwaongezea uzalendo kwa nchi yao.

Naye Mariam Salumu, mwanafunzi wa kozi ya Teknolojia ya uzalishaji wa sukari wa Chuo cha Sukari cha Taifa, akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa chuo hicho alisema kuwa wamefurahishwa na ziara hiyo kwa kuwa wamepata fursa ya kujifunza kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini hususani kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi hivyo watakuwa walinzi na mabalozi wa kutangaza rasilimali hizo.

 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...