Watu wanne wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Mkambalani wilayani Morogoro ikihusisha basi la abiria kampunu ya happy Nation lenye namba za usajilu T 702 DGF likilokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Jijini Mwanza kugongana uso kwa uso na Roli la mizigo lenye namba za usajili T179 DCR lililokuwa likitokea Zambia kuelekea Dar es salaam
Mkuu wa upelelezi mkoa wa Morogoro ACP Ralph Meela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo chanzo cha ajali kinadaiwa na uzembe wa dereva wa basi hilo Hassan Abdalah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lingine (overtake) bila kuchukua tahadari na kusababisha ajali hiyo
Mashuhuda wa ajili hiyo walisema dereva alikua anajaribu kuyapita magari mengine nane ndipo alipoashindwa na kijikuta anaingia upande ambao sio wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...