Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WATENDAJI wa kata za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuhamasisha zoezi la kampeni ya kitaifa ya chanjo ya UVIKO-19 itakayofanyika kwa siku 10 jijini hapa.

Kauli hilo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method katika kikao na watendaji wa kata kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Dkt. Method alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanza kutekeleza kampeni ya kitaifa ya chanjo ya UVIKO-19 inayolenga kuhamasisha uchanjaji kwa wananchi. “Dodoma Jiji tunatakiwa kuchanja watu 81,000 katika siku 10 za kampeni ya kuhamasisha kuchanja chanjo ya UVIKO-19. Kata moja itakuwa na timu zisizopungua nne na kila timu moja inatakiwa kuchanja watu 50” alisema Dkt. Method.

Mganga mkuu huyo aliwataka watendaji kuzisimamia timu hizo ili ziweze kufikia malengo kwa ufanisi. “Watendaji mkasimamie hizo timu ili zoezi liweze kufanikiwa. Mtendaji hakikisha kila siku wenye vituo wanakwambia wamechanja watu wangapi.

 Fuatilieni timu zinazoshiriki zoezi la uchanjaji. Pateni taarifa za uchanjaji kila siku jioni ili kuona hali halisi ya uchanjaji na namna ya kuongeza nguvu na mikakati ya kuhamasisha ili kufanikisha zoezi la uchanjaji siku inayofuata” alisema Dkt. Method.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma lina kata 41 na mitaa 222 inayotekeleza kampeni ya chanjo dhidi ya UVIKO-19


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...