Meneja Msaidizi Masomo ya Muda Mfupi, Chuo cha BoT, Bi. Tulla Mwigune, akitoa elimu kuhusu historia ya sarafu zinazochapichwa na BoT kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Beroya walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Mabenki Mwandamizi, Bw. Gideon Rwegoshora, akifafanua jambo kuhusu BoT inavyosimamia wa sekta ya fedha nchini kwa mwananchi aliyetembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Sheria kutoka BoT, Bw. Ramadhani Myonga, akifafanua jambo kuhusu Dawati la Utatuzi wa Matatizo ya Wateja wa Huduma za Kibenki kwa mwananchi aliyetembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benki Kuu).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...