Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuhakikisha wanadumisha Amani iliyopo Nchini ili Serikali iweze kuleta maendeleo kwa Wananchi wake kama ilivyokusudiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo wakati akisalimiana na Waumini wa Masjid TAQWA uliopo BAMBI BRANJI Wilaya ya KATI Mkoa wa Kusini Unguja mara baada ya kumalizika Sala ya Ijumaa.
Amesema ni vyema kuendeleza kudumisha Amani iliyopo pamoja na kuiombea Nchi na Viongozi wake ili Serikali iweze kutekeleza ahadi zake za kimaendeleo ambayo imejipangia kuwafanyia Wananchi wake wa Zanzibar kwa kizazi cha sasa na cha baadae.
Mhe. Hemed amewahakikishia wananchi wa Bambi na Wazanzibari kwa ujumla kuwa Serikali inayoongozwa na Dkt. Mwinyi itahakikisha inawapatia Wananchi wake Huduma zote muhimu za kijamii ikiwemo ujenzi wa Miundombinu ya Barabara kwa kiwango cha Lami, Hospitali, Skuli, Maji safi na salama na mengineyo ili kuwarahisishia Wananchi wake kujipatia huduma hizo.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Viongozi Wakuu wa Nchi kwa lengo la kuiongoza vyema Zanzibar kwa Busara na Uadilifu ili waweze kuwatumikia wananchi wake.
Akigusia suala la Mashirikiano ndani ya Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka Waumini wa bambi na maeneo mengine kuwaombea dua wale wote waliokuwa hawaelewi na kubeza maendeleo waweze kuelewa Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kuijenga zanzibar yenye maendeleo
Pia Alhajj Hemed amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anatumia nafasi aliyokuwa nayo katika kuijenga Zanzibar na Serikali itaendelea kuyatekeleza yale yote ambayo imeyaahidi kwa wananchi wake.
Kwa upande wake Sheikh JUMA ALI HASSAN katika Khutba ya Sala ya Ijumaa amewataka Waumini kuongeza uaminifu kwa Viongozi na kudumisha Amani iliyopo Nchini kwa lengo la kupata maendeleo yanayoletwa na Viongozi wetu kwa maslahi ya wazanzibari wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...