Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Lubinga Ngemela akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jukwaa la Vijana Wanasiasa Tanzania (WAVITA) waliotembelea Ofisi Ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Lumumba Jijini Dar es Salaam

*Kuzunguka nchi nzima kuainisha fursa za ajira kwa vijana katika maeneo yao

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
JUKWAA la Vijana Wanasiasa Tanzania (WAVITA) limesema kuwa halitaki kuona vijana kuwa sehemu ya walalamikaji wa mifumo ya serikali badala yake wanakuwa vijana wawajibikaji kwa kutumia fursa zilizo katika maeneo yao.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa WAVITA Shiganga George mara baada kutoka kutambulisha uongozi jukwaa hilo kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) katika Ofisi ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika kutengeneza fursa za vijana kuwajibika wanakwenda kutoa elimu kwa vijana nchi nzima kwa kuwabadilisha kufanya kazi kwenye maeneo yao na kuweza kuzalisha vitu mbalimbali na kujipatia kipato na kuchangia maendeleo ya nchi.

George amesema katika kufanya kazi hiyo watafanya kazi bila kujali itikadi ya vyama lengo ikiwa nj kutaka vijana wafanye kazi kwani kulalamika huko inatokana na kutokuwa na kiti cha kufanya.

Aidha amesema vijana kwa sasa wana elimu ambapo wanakwenda kuonyesha namna ya elimu watavyoweza kuitumia katika kuzalisha kwenye maeneo yao na suala la mitaji serikali imeweka mifumo kupitia katika halmshauri kutenga bajeti kwenye makundi mbalimbali ikiwemo na vijana.

Amesema vijana wamekuwa wanaangalia vyeti badala ya kuangalia fursa za uwajibikaji

Muasisi na Vijana na Mlezi na Msemaji William Machimu amesema kuwa katika safari kwenda ofisi ndogo za CCM ni kupekeleka salamu kwa Rais Samia Hassan Suluhu kwa kazi anayofanya katika kukuza Demokrasia pamoja na kujenga uchumi wa nchi na salamu za pili ni pongezi kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdullahman Kinana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...