Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana akipata maelezo kutoka kwa Afisa Muhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kassim Ramadhan wakati Waziri alipotembelea Banda la TFS katika maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kufanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana akipokea zawadi ya Asali kutoka kwa Kamishina Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Profesa Donsatos Silayo wakati Waziri alipotembelea Banda la TFS katika maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kufanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana akipata maelezo kutoka kwa Kamishina Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Profesa Donsatos Silayo wakati Waziri alipotembelea Banda la TFS katika maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kufanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Kamishina Mkuu Profesa Silayo amuahudi Waziri kuendelea kuwa wasimamizi wa uhifadhi wa misitu
Na Chalila Kibuda, Muchuzi Tv
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana amewapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kwa kazi wanayofanya katika kuhifadhi misitu na rasimali za misitu.
Aliyasema hayo wakati alipotembelea banda la Maliasili na Utali kwenye maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa misitu ndio chanzo cha upatikanaji wa maji ambayo ndio uhai hivyo kunahitaji usimamizi dhabiti katika misitu.
“Leo tumeona masuala ya misitu, hili ni eneo mojawapo ambalo ni muhimu tunalopaswa kulitunza ili tuweze kunufaika sote, tunapotunza misitu, vyanzo vya maji na nishati vinakuwa salama, leo hii tunapoingiza Wanyama tunahatarisha vyanzo vyetu vya maji, nitowe wito kwa wafugaji tuone maeneo yapi yanafaha kufugia na tusifuge maeneo ya hifadhi,
Amesema haabari ya moto katika maeneo ya misitu tunazo sheria na miongozo yakufuata inayoeleza ni namna gani unavyoweza kuanzisha moto pindi unapotaka kuanzisha moto kwa ajili ya kusafisha mashamba bila kusababisha uharibifu wa misitu yetu, ni lazima tutunze misitu”amwsema Mhe.Chana
Balozi Chana amesema kuwa licha kuendelea kusimamia misitu wananchi wanatakiwa kuwa sehemu ya ulinzi kwa kufanya shughuli zingine ikiwemo ufugaji wa nyuki ambao unawapatia asali na kuuza hivyo maisha yao yanakwenda bila kukata misitu.
Kwa upande wa Kamishna Mkuu wa Misitu Profesa Dosantos Silayo amesema kuwa shughuli wanazofanya wanashirikisha wadau mbalimbali katika kuhakikisha misitu inatunzwa na kufanya rasilimali misitu kuwa yenye tija.
Profesa Dosantos amesema kazi kubwa wanayoifanya ni kutoa huduma kwa wadau ili iwe na tija kwao kwa kuzalisha bidhaa na kuuza kwa kushirikiana na wadau ambao wanafanyakazi ambazo zinachangia kwenye uhifadhi wa rasilimali nyuki.
Kwa upande wa Afisa Muhifadhi Kassim Ramadhani ameeleza kuwa TFS imetenga maeneo maalum ya mikakati kwa ajili ya kupanda mbegu bora za miti katika vituo vya Morogoro,Lushoto,Iringa kwa ajili ya kuwafikia wananchi mbalimbali.
Aidha amesema katika kuhakikisha miti inakua na tija wamekua na wadau ambao wanazalisha asali na Nta kwa kufuga nyuki.
"Katika ufugaji wa nyuki,tumewaandaa wadau wanaozalisha mazao ya nyuki wanaongeza thamani ya mazao na kuuza kwenye masoko mbalimbali ambao nao wameshiriki maonesho ili waweze kupata masoko mengine"amesema Kassim.
Amesema TFS pia inafanya shughuli za Utalii wa Ikolojia ambao unafanyika kwenye maeneo ya misitu na msimu huu tayari wameshatembelewa na wageni 152,000 katika msimu huu ambao umeisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...