Na Kijakazi Abdalla
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaomba mashirika ya Marekani kuisaidia Zanzibar katika kuwapatia vifaa na elimu ya afya ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto ifikapo mwaka 2030.
Waziri Mazrui ameyasema hayo huko Ofisi kwake Mnazimmoja wakati akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright.
Aidha amesema Zanzibar inatarajia kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuhakikisha ina kuwa na uzazi wa mpango kwa kina mama ili kuzaa watoto wa wenye afya na siha.
Vilevile amesema kutokana na changamoto hizo wizara inajenga hospitali za Wilaya na Mkoa ambazo zitakuwa na sehemu maalum ya akinamama na watoto ambapo kutawezesha kupunguza vifa vitokanavyo na uzazi.
Hata hivyo amesema Wizara ya Afya wataanza kupita nyumba kwa nyumba ,masokoni na sehemu mbalimbali katika kampeni ya chanjo ya uviko 19.
Vilevile Waziri Mazru amesema kupitia jitihada za Serikali na wadau mbalimbali wanaosaidia katika sekta ya afya zimewea kupunguza kwa kiasi kikubwa mradhi ya malaria na HIV.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright ameeisifu Wizara ya Afya kwa jitihada za kupunguza maradhi ya uviko 19 Zanzibar pamoja na maradhi ya malaria.
Aidha amuhakikishia Waziri wa Afya kwa kupitia Serikali yake ya Marekani itahakisha Zanzibar inaondikana na changamoto mabalimbali za maradhi.
“Tutazidi kuunga mkono Serikali ya Zanzibar ili kuhakikisha tuondosha changamoto za maradhi”alisisitiza Balozi Donald Wrght.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe .Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald Wright na ujumbe wake walipofika Ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali yatakayopelekea kukua kwa sekta ya Afya Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dkt Donald Wright wakati alipfika Ofisini kwake kwaajili ya kujadiliana mambo mbalimbali yatakayopelekea kukua Kwa sekta ya Afya Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...