Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Leonard Mkude, akisikiliza maelezo kuhusu Idara ya Uchambuzi wa Sera kutoka kwa Mchumi Bw. Fronto Furaha, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF Bw. Ekwabi Mujungu akipokea fomu ya kujiunga uanachama Hazina-Saccos kutoka kwa Afisa Mikopo Bi. Bakita Malongo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), jijini Dar es Salaam.
Mchumi kutoka Idara ya Mipango ya Kitaifa, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Irene Mghase, akitoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya Mipango ya Kitaifa walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), jijini Dar es Salaam
Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Leonard Mkude, akitoa pongezi kwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati alipotembelea Kitengo cha Pensheni na Mirathi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango - Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...