Na Said Mwishehe, Michuzi TV 
 SHIRIKA la Bima la Taifa(NIC) leo Julai 7,2022 katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam limeendelea kuelezea majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Shirika hilo katika kuwahumia Watanzania. 
Hata hivyo kutokana na ukubwa na umuhimu wa Shirika hilo hasa katika eneo la bima, viongozi wa Serikali, wakuu wa idara, taasisi na mashirika ya umma na binafsi ni miongoni mwa waliopita kwenye banda la NIC kwa ajili ya kupata maelezo yaliyokuwa yakitolewa na maofisa washirika hilo.  
Miongoni mwa viongozi waliofika banda la NIC ni pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko aliyetumia muda wake mwingi kupata maelezo kutoka kwa maofisa wa shirika hilo ambapo kwa sehemu kubwa ameoneshwa kufurahishwa na kazi zinazofanywa na NIC. Wakati akiwa katika banda hilo Dk.Mafumiko alikuwa akiongozwa na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko wa NIC Yesaya Mwakifulefule. Mwisho 
Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa(NIC) Yesaya Mwakifulefule(katikati) akifafanua jambo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Dk.Fidelice Mafumiko(kulia) baada ya kufika kwenye banda la shirika hilo leo Julai 7,2022.
Ofisa wa Shirika la Bima la Taifa(NIC) Elizabeth Chacky akielezea jambo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko baada ya kutembelea banda la shirika hilo.Wa pilia kulia ni Mkurugenzi wa Masoko NIC Yesaya Mwakifulefule.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko (kushoto) akipata maelezo kuhusu shirika hilo kutoka kwa Elizabeth Chacky.
Dk.Fidelice Mafumiko ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali(kulia) akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la NIC.
Ofisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi katika Shirika la Bima la Taifa(NIC) Alex Suzuguye(kushoto) akizungumza jambo wakati Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fedilice Mafumiko (kulia).
Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko(katikati) akieleza jambo kwa maofisa wa Shirika la Bima la Taifa.
Elizabeth Chacky kutoka Shirika la Bima la Taifa(NIC) akikabidhi moja ya jarida la shirika hilo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko(katikati). Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko Yesaya Mwakifulefule.
Mkurugenzi wa Masoko NIC Yesaya Mwakifulefule (kushoto) akieleza jambo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fedilce Mafumiko (katikati) na kulia ni ofisa wa shirika hilo Elizabeth Chacky.
Mkurugenzi wa Masoko NIC Yesaya Mwakifulefule(katikati) akifafanua jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...