Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe

Jeshi la polisi Mkoani Pwani linamshikilia mtu mmoja mwanaume miaka 32 msanii na mkazi wa Sanze kata ya Kisarawe wilaya ya Kisarawe ,akiwa na silaha bandia za kivita Ak smg 11,uzgun moja ,pisto 5, vest za kukinga risasi mbili zilizotengenezwa kwa plastic na mbao na redio calls bandia.

Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,Pius Lutumo akizungumza na waandishi wa habari, ameeleza mtu huyo amekamatwa kupitia taarifa fiche.

Lutumo ameeleza, katika mahojiano na mtuhumiwa amekiri kuwa anatengeneza silaha hizo na anatumia kwa matumizi yake na kuupelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Sambamba na hayo Kamanda huyo ametoa wito kwa jamii kuishi kwa kufuata misingi ya sheria kama wanahitaji kutumia silaha kwa namna yoyote,na wafuate sheria na taratibu zilizowekwa za kupata vibali toka Taasisi husika.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...