Na John Walter-BabatiMwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahmani Kololi ameiagiza Halmashauri hiyo kuwaondoa mbwa wanaozagaa mtaani ovyo kwa kuwaua.

Amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa mbwa hao wamekuwa kero na wakati mwingine kung'ata watu hali inayowapa hofu.

Akizungumza katika baraza la madiwani,Kololi amesema mitaa inayoongoza kwa kuwa na mbwa wengi wanaozurura ni mjini Babati na Bagara.
Mwaka 2017 Jumla ya Mbwa 347 kati ya zaidi ya 3600 wanaozurura mitaani katika mji wa Babati waliuawa kwa kupigwa risasi na Idara ya mifugo ya Halmashauri hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...