*Ni baada ya kudaiwa kuwa chanzo cha kukwamisha usajili wa vyama vya msingi kwa wakulima
Na Mwandishi Wetu, Tabora
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka
amemuagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuondoa haraka Mrajisi wa
Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora kwa madai amekuwa chanzo cha
kukwamisha jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua
wakulima wa zao la tumbaku na kusaabisha malalamiko kwa wakulima wa
mkoa huo .
Shaka ametoa maagizo hayo leo Agosti 19,2022 wakati
alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ufumula wilayani Uyui
mkoani Tabora ambapo akiwa hapo alipokea malalamiko mbalimbali ya
wakulima wa zao tumbaku na miongoni mwa malalamiko ni ya kuwepo kwa
urasimu wa kusajiliwa vyama vya msingi(AMCOS).
Akizungumza wakati
anatoa maagizo hayo Shaka amesema amepokea malalamiko ya Mrajisi wa
vyama vya ushirika mkoa wa Tabora Geophrey Chiliga kuwa na changamoto
mbalimbali zinazokwamisha jitihada za wakulima. “Changamoto za bwana
huyu imekuwa donda sugu , tumetoka Kaliua analalamikiiwa, tumetoka
Sikonge analalamikiwa, tumetoka Urambo analalamikiwa, leo tuko Uyui watu
wanalia na huyu bwana. Urasimu umekuwa mkubwa sana.
“Utitiri na
ukiritimba umekuwa mkubwa sana kiasi unadumaza jitihada na huko
tunakotoka hajasajili vyama kwasababu kuna mawakala wanapita chini kwa
chini , Mbunge kasema na mimi taarifa ninazo wako mawakala wanapita
chini kwa chini kuwaambia wakulima nenda kajiunge pale. Yeye sio kazi
yake , yeye sio jukumu lake la nani akajiunge ushirika gani .
“Nani
ahame wapi na aende wapi, hiyo sio kazi yake hapa kuna vyama vya
ushirika 18 havijasajaliwa , amesajili saba tu na hivyo saba kwasababu
ya mawakala wake na inaonekana kuna mazingira ya rushwa yanatengenezwa
wakati Serikali inapiga vitaa”amesema Shaka na kuongeza ujanja ujanja
huo unaonekana kuna baadhi ya watu wanajitengenezea kipato ambacho sio
halali kupitia jasho la wakulima wa tumbaku.
“Maelekezo yetu kwa
Wizara ya Kilimo kupitia Waziri wa Kilimo amuondoe mara moja huyu
Mrajisi wa vyama vya ushirika , narudia tena maelekezo kwa Waziri wa
Kilimo amuondoe, kwasababu Tabora ndio inaongoza kwa kilimo cha tumbaku
hivyo hawawezi kuona jitihada za Rais Samia anatokea mtu mmoja tu
anazikwamisha halafu bado akaendelea kuchekewa,”amesema Shaka.
Amesisitiza
Waziri wa Kilimo watamjulisha kwamba Mrajisi huyo hafai kuwa Tabora na
hivyo wampangie majukumu mengine sehemu ambayo hakulimwi kilimo cha
tumbaku aende akafanye anavyotaka lakini sio Tabora. Tutalinda jasho
lenu lakini tutalinda jitihada za Rais Samia anazoziweka ili kukuza zao
hili la tumbaku,”alisema Shaka.
Amesema zao la tumbaku
linawaheshimisha wana Tabora, limekuwa mkombozi kwao na Rais Samia
ameongeza ushindani katika ununuzi kutoka kampuni mbili mpaka kampuni
sita halafu, halafu anatoa mjanja mmoja anataka kukwmaisha jitihada hizo
na CCM hakiwezi kukubali , hivyo watalala naye mbele.
Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamebeba bango la kumkaribisha mgeni wao

Katibu wa nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipiga Ngoma baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfuluma, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani ya I chaguzi ya CCM ya 2020-2025. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...