Njombe

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe limeagiza kuteketezwa kwa nyavu haramu zote zitakazokuwa zinakamatwa katika ziwa Nyasa kwa kuwa zimekuwa na madhara makubwa kwa wananchi na kuathiri uchumi na viumbe hai.

Katika mkutano wa baraza la madiwani wilayani humo baadhi ya madiwani akiwemo Chrispin Mwakasungura toka kata ya Makonde ameonesha masikitiko yake namna nyavu haramu zinazokamatwa na kurejeshwa tena ziwani kwa njia za udanganyifu jambo analosema linasababisha kukosa ubora wa samaki na hata kulikosesha mapato taifa kwa kuwa zilizo nyingi zinaingizwa nchini kwa njia za magendo.

Mwenyekiti wa kamati ya uchumi ujenzi na mazingira ambaye ni Diwani wa kata ya Milo Bwana Robert Njavike amesema zoezi la kukamata nyavu haramu na kuziteketeza limeendelea kufanyika mwambao mwa ziwa nyasa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias ametumia fursa hiyo kuwaonya maofisa watendaji wa vijiji na kata wanaohudumu mwambao mwa ziwa nyasa na kuwataka kuacha kutumika vibaya pindi wanapokamata nyavu hizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bwana Wise Mgina amesema kumekuwa na ujanja ujanja mwingi pindi nyavu haramu zinapokamatwa kitu ambacho hakipaswi kufumbiwa macho.

Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa makubwa nchini Tanzania ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii pamoja na kuwapatia kipato wananchi kwa kuvua samaki.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...