Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha billioni 16 kwa mwaka uliopita wa fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mpwapwa.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. George Simbachawene katika mapokezi ya mbio za mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.  Wenye kauli Mbiu “sensa ni Msingi wa Mpango wa maendeleo. Shiriki kuhesabiwa  tuyafikie maendeleo ya Taifa.”

“Watu wanahitaji kusikia shida zao zinazungumzwa, ni imani yangu kwamba viongozi tutaendelea kushirikiana na fedha yoyote ya mradi wa maendeleo itakayokuja tutaitumia vizuri”

Waziri Simbachawene amepongeza timu ya wakimbiza Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kufanya kazi nzuri. Mwenge wa uhuru umekimbizwa kwa umbali wa km 100 na umezindua miradi miwili, miradi mingine miwili imewekwa jiwe la msingi na mradi mmoja kutembelewa yenye thamani ya zaidi billion 1.4



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...