KAMPUNI zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani, tayari zimethibitisha kushiriki katika maonesho makubwa ya famasia yanayofahamika kama ‘Pharmatech East Africa’ yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam, ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 30-1 Septemba, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Wafamasia nchini [PST], Fadhili Hezekiah wakati wa warsha iliyohusu uelewa wa chama hicho na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam, Ambapo amesema kuwa maandalizi yameshakamilika na hadi sasa tayari kampuni hizo zimethibitisha.

‘’Maonesho haya ni mahususi na muhimu kama Taifa kuweza kujitokeza kujionea kujifunza kwani ni ya kwanza na ya kipekee kwa Tanzania hasa sekta ya afya.

Tunategemea kuwa na kampuni zaidi ya 100, lakini hadi sasa kampuni 60 tayari zimethibitisha, hii ni hatua kubwa sana kwetu kama waandaji kwa ushirikiano na kampuni ya ETSIPL.’’ Alisema Rais wa PST, Fadhili Hezekiah.

Aidha, amewaomba wadau na watu mbalimbali ikiwemo Vyuo vya Famasia nchini, kujitokeza kwa wingi kujionea maonesho hayo kwani ni sehemu ambayo watajifunza na kupata mashirikiano.

‘’Maonesho haya yanakuja na vitu mbalimbali. Makampuni yataonesha bidhaa zao ikiwemo dawa, na vifaa tiba, tutaona dawa kuanzia hatu ya awali hadi inapokuja kuwa dawa…kutakuwa na vitu zaidi kutoka kwenye makampuni haya makubwa duniani, ikiwemo Bara la Ulaya, Asia na kwingine,

Tunaomba makundi mbalimbali waje na wajifunze na hata kuona namna ya kuwekeza sekta ya dawa’’ alisema Rais wa PST, Fadhili Hezekiah.

Kwa upade wake, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL ya maonesho ya kibiashara kutoka India, Bw. Digvijay Singh ambao wanafanya maonesho hayo kwa kushirikiana na PST, amesema kuwa, Tanzania imekuwa na bahati kubwa, kwani makampuni makubwa yanakuja kuonesha bidhaa zao ambapo itachagiza fursa za uwekezaji.

‘’Kampuni kubwa kutoka nchi kama India, Uganda, Misri, Kenya, Rwanda na nyingine nyingi Bara la Ulaya, zinakuja kuonesha bidhaa zao, dawa na vifaa tiba, ambapo pia itakuwa ni fursa za wao kuwekeza hapa nchini, hivyo wadau na watu mbali mbali waje waone ni bure kabisa’’ alisema Singh.

Aidha, maonesho hayo pia yanawezeshwa na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kupitia Wizara ya Afya, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba [TMDA], Bohari kuu ya Dawa [MSD] na wengine wengi.


Rais wa Chama cha Wafamasia nchini (PST) Fadhili Hezekiah akifafanua mambo mbalimbali mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), leo Agosti 25,2022 jijini Dar es Salaam kwenye warsha iliyohusu uelewa wa majukumu mbalimbali ya chama hicho kwa Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL ya maonesho ya kibiashara kutoka India, Bw. Digvijay Singh akieleza jambo wakati wa warsha iliyohusu uelewa wa Chama cha Wafamasia kwa Waandishi wa Habari,leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Afya Bi.Catherine Sungura alipokuwa akiwakaribisha Waandishi wa Habari kwenye Warsha fupi ya iliyohusu uelewa na majukumu ya Chama cha Wafamasia iliyofanyika leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Afya Bi.Catherine Sungura akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL ya maonesho ya kibiashara kutoka India, Bw. Digvijay Singh wakati wa warsha iliyohusu uelewa wa Chama cha Wafamasia kwa Waandishi wa Habari,leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam.



Pichani juu baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...