CHAMA cha Wafamasia nchini kimesema wao kama Wafamasia wakiwa kwenye famasi zao au katika maeneo ya hospitali wanayo nafasi ya kuwakumbusha watu kuhusu mtindo wa maisha unaoweza kusababisha magonjwa sugu.
Aidha kwa kufanya hivyo watakuwa wametatua tatizo kwa maana ya kuzuia watu wasiingie kwenye magonjwa sugu au kama yapo tayari yameshamnyemelea mtu basi watakuwa wamepunguza madhara makubwa yanayoweza kupatikana.
Hayo yameelezwa leo Agosti 25,2022 na Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Fadhili Hezekiah wakati wa semina iliyoandaliwa na Chama hicho kwa waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali nchini.
Pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua kuhusu muundo na majukumu ya Chama hicho huku akielezea umuhimu wao katika jamii hasa kwa kuzingatia Wafamasia ni kundi la watalaamu ambao linafika kwa urahisi na kutatua changamoto za watu.
Akizungumzia kuhusu matumizi sahihi ya dawa, amesema Wafamasia ni watu ambao wako kwenye nafasi nzuri sana wakitumika vizuri kuweza kusaidia umma katika kutumia dawa kwa mtazamo sahihi.
“Lakini pili kuna changamoto kubwa kutokana na matumizi ya dawa yanayosababisha usugu wa dawa, kwa hiyo Chama cha Wafamasia kupitia wanachama wake tunaamini tunayo nafasi kubwa ya kutoa elimu kuhusu matumizi yote ya dawa.
“Kwa hiyo tunazo Kamati kama ya wanachama, kamati ya mipango, kamati ya elimu ambayo ndio msingi katika kutoa elimu ya famasia na tunayo kamati ya maadili na katiba ambayo inatusaidia sana pale ambapo tunakengeuka ili kusaidia kutuweka sawa katika kuboresha utendaji kazi wetu, pia tunazo kamati zinazoweza kutokea kulingana na matukio,”amesema Hezekiah.
Aidha amesema nia yao ni kuhakikisha wanachangia katika uwezekano wa kutoa huduma za afya na hapo unaangalia eneo la upatikanaji wa dawa hasa bajeti ya dawa kwa kuanzia asilimia 60 na kuendelea katika maeneo ya vituo vya afya na sekta ya afya.
“Kwa hiyo katika mazingira kama hayo kwasababu sisi ni watalaamu wa dawa basi tunajikuta kwamba tunaangalia katika eneo hili, tukitumia uwezo wetu vizuri tunaweza kusaidia upatikaji wa dawa, na hapo ni watu wote iwe dawa bora, dawa salama na ipatikane wakati inapohitajika kwa bei isiyo ngumu kwa kila mtu.
“Lakini pia kuna changamoto sasa tumeanza kuiona inatokea kwenye masuala ya ongezeko la magonjwa sugu au magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza, magonjwa haya mengi tunachelewa kuja kutatua kwasababu hayana zile athari nzito za haraka.
“Sio kama magonjwa ya kipindipindu ambapo dalili zake zinaonekana, lakini kama ugonjwa wa sukari utachukua muda kugundua na hasa kama mtu hana tabia ya kuchunguza afya.
“Sasa kwanini tunasema famasia anaweza kuwa katika nafasi nzuri kusaidia kwenye mapambano. Ni kwasababu tafiti zimefanyika na kuonesha wafamasia pamoja na famasi kwenye ngazi zake zote ambazo zipo wapo rahisi kufikika, ”amesema.
Pichani juu baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
Rais
wa Chama cha Wafamasia nchini (PST) Fadhili Hezekiah akifafanua mambo
mbalimbali mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), leo Agosti
25,2022 jijini Dar es Salaam kwenye warsha iliyohusu uelewa wa majukumu
mbalimbali ya chama hicho kwa Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL ya maonesho ya kibiashara kutoka
India, Bw. Digvijay Singh akieleza jambo wakati wa warsha iliyohusu
uelewa wa Chama cha Wafamasia kwa Waandishi wa Habari,leo Agosti 25,2022
Jijini Dar es Salaam
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Afya
Bi.Catherine Sungura alipokuwa akiwakaribisha Waandishi wa Habari kwenye
Warsha fupi ya iliyohusu uelewa na majukumu ya Chama cha Wafamasia
iliyofanyika leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Afya
Bi.Catherine Sungura akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
ETSIPL ya maonesho ya kibiashara kutoka India, Bw. Digvijay Singh wakati
wa warsha iliyohusu uelewa wa Chama cha Wafamasia kwa Waandishi wa
Habari,leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...