Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2022 wakati akitoa taarifa ya utendaji wa Mfuko pamoja na vipaumbele vya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2022.

*Mkurugenzi Mkuu ampongeza Mama Samia kwa kuwa chachu la ongezeko la wawekezaji

Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amesema Mfuko umepata matokeo makubwa na mazuri ya uwekezaji kutokana na kuwekeza kwenye maeneo salama.

Mshomba amesema hayo jana jijini Dar es Salaam leo Agosti 19,2022 wakati akitoa Taarifa ya Utendaji wa Mfuko pamoja na Vipaumbele vya Mfuko kwa mwaka wa Fedha 2022/23.

Amesema katika kipindi cha miaka miwili uwekezaji umeleta mapato makubwa ambayo hayajawahi kufikiwa kwani NSSF haikuweza kupata mapato ya mwaka zaidi ya Shilingi bilioni 500, lakini katika mwaka huu wa fedha wamepata zaidi ya Shilingi bilioni 600.

Amesema matokeo hayo ya uwekezaji yametokana na Mfuko kujikita zaidi katika uwekezaji kwenye maeneo ambayo yanaleta faida kwa Mfuko na kuhakikisha wanaudhibiti wa fedha.

Mshomba amesema chachu kubwa ya mafanikio ya NSSF yamechagizwa na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi makini wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu amekuwa chachu ya ongezeko kubwa la wawekezaji hapa nchini hususan katika sekta binafsi.

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa chachu ya mafanikio ya Mfuko wetu kutokana na kufungua fursa za uwekezaji." alisema.

Kuhusu waajiri kutowasilisha michango alisema wameweka mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ili kupata orodha kamili ya waajiri ambao watawafikia na kufuatilia michango ya wanachama.

Mshomba amewahamisha Watanzania wote kushiriki katika zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo tarehe 23 Agosti, 2022 ili waweze kuhesabiwa.

Hata hivyo amesema Mfuko wa umepata mafanikio makubwa na umekuwa kwa kasi kubwa.

"Tumepata mafanikio makubwa katika suala zima la ukuaji wa Mfuko na hii imesababishwa na sababu kadhaa ikiwemo kuweka misingi imara na madhubuti ya ukusanyaji wa mapato," alisema.

Mshomba amesema ukuaji huo ni mkubwa tofauti na miaka miwili ya nyuma iliyopita ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa ni Shilingi Trilioni 4.3 na kuwa ukuaji huo umechangiwa na ongezeko la mamusanyo ya michango.

Amesema katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022, Mfuko ulikusanya zaidi ya Shilingi Trilioni 1.42 kwamba makusanyo hayo ni zaidi ya hata bajeti ambayo walijipangia iliyokuwa Shilingi Trilioni 1.38.

Mshomba amesema pia Mfuko umeboreshaji sana udhibiti wa matumizi jambo ambalo limechangia ukuaji wa NSSF.

Mafanikio mengine yaliyopatikana, amesema ni uboreshaji wa huduma hasa kwa kutumia mifumo mbalimai ya TEHAMA ambapo sasa mwanachama na wadau wanaweza kupata huduma popote walipo bila ya kufika katika ofisi za NSSF kwa kutumia mifumo ya Employer Potal na Member Potal.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...