Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James  akizungumza na viongozi mbalimbali wa Taasisi zisizo za kiserikali jijini Dar es Salaam leo Agosti 26, 2022.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi zisizo za kiserikali jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya viongozi wa NGO's wakiwa kwenye kikao leo jijini Dar Es Salaam leo.

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amewaasa taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) zilizopo katika wilaya ya Ubungo kufanya majukumu yao bila kuvunja sheria na taratibu za nchi.

Ameyasema hayo leo Agosti 26, 2022 wakati akifungua Kikao cha Viongozi wa Asasi zisizo za kiserikali jijini Dar es Salaam. Amesema  Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan anawategemea na Serikali inawategemea katika ufanyaji wa shughuli zao.

Viongozi wa Mashirika hayo wamekutana leo kwa lengo la kujadiliana na kuwasilisha taarifa za mwaka zikiwemo taarifa za miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa.

James amesema anatamani kuona mashirika hayo yasio ya kiserikali yanatoka maofisini na kushirikiana na wananchi moja kwa moja kuliko kujifungia ndani. 

Aidha  amewataka Viongozi wa Mashirika hayo yasiyokuwa ya Kiserikali kufanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa Maendeleo wa Wilaya ya Ubungo ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Licha ya hayo amewaasa kuwa wazalendo katika ufanyaji wa shughuli zao hata kama wanasaidiwa na taasisi za kutoka nje ya nchi.

Kwa Upande wa Katibu wa  Baraza linalosimamia changamoto za taasisi zisizo za Kiserikali, Joseph Yohana amesema kuwa taasisi hizo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukosa wadau wa maendeleo na kukosa maeneo ya kufanyia shughuli zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...