RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbili.

Katika taarifa iliyotelewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus leo Agosti 25, 2022 imeeleza kuwa Rais amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Damian Lubuva ambaye alimaliza muda wake.

Pia amemteua Prof. William Andey Lazaro Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Prof. Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.

Amesema uteuzi huo umeanza  Agosti, 23 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...