Na Oscar Assenga,TANGA.
RAIS Samia Suluhu anatarajiwa kuwasili kesho mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya siku mbili mkoani Tanga ambapo akiwa mkoani hapa atazindua Chuo cha Jeshi la Uhamiaji cha Taifa.
Akizungumza leo wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema Rais Samia ataingia mkoani Tanga kesho mchana na Jumatatu atafanya ziara wilayani Mkinga
Mgumba alisema Rais Samia atazindua chuo hicho cha Jeshi la Uhamiaji kilichojengwa eneo la Boma KichakaMiba wilayani Mkinga ikiwemo kufunga mafunzo ya wanajeshi wa jeshi jipya la Uhamiaji zaidi ya 818 waliohitimu mafunzo.
Alisema baada ya Rais Samia ataondoka ambapo pia alitoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumlaki katika maeneo yote atayopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...