
UNAPOKUWA katika wakati mgumu, unafaa kuwa na matumaini kuwa kuwa jamii yetu ni bora sana, na changamoto zako sio za kwako peke yako. Andrew Rossi, alifarijika sana kuona nyuso za wana Meridianbet wakigonga hodi nyumbani kwake.
Bwana Rossi, ana changamoto ya kiafya,
ambayo alihitaji kiasi cha fedha kwa ajili ya vipimo vya afya na matibabu.
Timu ya Meridianbet, ikiwa pamoja na
mmoja wa mabalozi wake Jackob Mbuya, waliwasili nyumbani kwa bwana Rossi, baada
ya kupata taarifa zake za kuugua na uhitaji.
Kupitia programu yao ya “Shinda Penati
Uisaidie Jamii Yako”, ambayo mabalozi na wahamasishaji wanakaribishwa kupiga
mikwaju ya penati, ambayo kila goli linalofungwa lina thamani ya shilingi elfu
hamsini, Mbuya aliweza kucheka na nyavu kwa mikwaju yote mitano aliyocheza.
Mbuya, alipewa nafasi ya kuchagua wapi
angependa kuielekeza pesa yake aliyoshinda kwenye mikwaju ya penati, ili
kuisaidia jamii inayomzunguka. Mbuya, alichagua kuelekeza kiasi cha ushindi
wake kwenye matibabu ya Mzee Andrew Rossi, mkazi wa Buza.
Meridianbet, waliongeza kiasi
cha laki mbili na nusu, kwenye laki mbili na nusu iliyopatikana kwenye mikwaju
ya penati kukamilisha kiasi cha laki tano, kilichofikia uhitaji wa vipimo na
manunuzi ya dawa ya mgonjwa, pamoja na mahitaji kadhaa ya nyumbani.
Mzee Andrew Rossi alitoa shukrani zake kwa Meridianbet “Nawashukuru sana
Meridianbet, naamini mungu atawaongeza pale walipopunguza, nimefarijika sana”
Meridianbet, ambao ni mabingwa
na wakongwe wa uendeshaji wa michezo ya kubahatisha Tanzania, wakiwa na
ubashiri wa michezo na kasino ya mtabdaoni, wanataja kuwa hii ni namna bora
kwao kuwa karibu na jamii yake.
“Naam, hii ni namna ambayo tumekuwa
tukiitumia kurejesha kwa jamii. Tunaona kuwafikia wazee na wahitaji wengine
kunatuweka karibu na jamii yetu. Tunafahamu hatuwezi kutatua changamoto zote,
lakini tunajitahidi kama hivi” – Dickson Richard, kutoka kitengo cha maudhui
cha Meridianbet.
Twaha Mohamed, kutoka kitengo cha Masoko
pia aliongeza kuwa “Kwa wapenzi wa ubashiri, licha ya ukweli kuwa wanajiweka
katika nafasi kubwa ya kushinda jackpot za Meridianbet Casino, pia
wanaiwezesha Kampuni hii kusaidia umma.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...