KAIMU Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bi. Josephine Bujiku ametoa wito kwa wananchi wote wanaotumia vyombo vya usafiri kwa njia ya maji kuhakikisha wanafahamu wajibu wao katika kuimarisha Usalama pindi wanapotumia Usafiri huo.
Akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la TASAC katika maonesho ya NaneNane Mkoani Mbeya Bi. Josephine aliwaasa wananchi kuzingatia maelekezo wanayopewa na Maafisa wa TASAC katika maeneo mbalimbali ya mialo ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazotokana na usafiri huo.
“Maafisa wetu wanatoa elimu mbalimbali kuhusu wajibu wa abiria katika mialo yetu hivyo nawashauri kuwa makini kusikiiza na kutekeleza yale yote mnayoelekezwa ili kujikinga na ajali pindi mtumiapo vyombo vya usafiri majini” alisema Bi.Josephine
Aidha aliongeza kuwa watumiaji wa usafiri kwa njia ya maji wana wajibu wa kukataa kuingia kwenye boti au meli anapohisi meli au boti imejaza abiria au mizigo kupita uwezo wake na kutoa taarifa TASAC, Polisi au katika uongozi wa Serikali ulio karibu.Pia aliwasisitiza kusikiliza na kutekeleza maelezo ya mhudumu wa boti au meli kuhusu jinsi ya kutumia vifaa vya kujiokolea na namna ya kujiokoa iwapo itatokea dharura pamoja na kusikiliza na kufuata maelekezo ya mhudumu wakati wa kuingia, kutoka na wakati wote wa safari.
Aidha alitoa wito kwa mwananchi kuhakikisha anatunza mazingira na taka zote zinawekwa katika vyombo vya kuhifadhia taka vilivyopo katika eneo la bandari au kwenye boti/ meli.TASAC inashiriki Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya ambapo kilele chake kinatarajiwa kuwa tarehe 8 Agosti, 2022 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa.
Kaimu Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Josephin Bujiku akitoa Elimu kwa wanafunzi waliotembelea Banda la TASAC katika Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani MbeyaAfisa Uhusiano Nicholaus Kinyariri akimhudimia mwananchi aliyetembelea Banda la Banda la TASAC katika Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Afisa wa TASAC Maulid Nsalamba akimhudimia mwananchi aliyetembelea Banda la Banda la TASAC katika Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...