Njombe


Wananchi wa Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kuwajengea kilabu kwa ajili ya pombe za kienyeji kutokana na maeneo yao kukosa huduma hiyo huku serikali ikipoteza mapato kwa watu wanaoshindwa kupata huduma katika vilabu vya watu binafsi.

Ombi hilo limetolewa na wananchi wa kijiji cha Ludewa mjini kwa mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga na kutishia mgomo wa kunywa pombe mpaka serikali itakapowasaidia kupata kilabu cha pombe za kienyeji.

“Wenzetu wote vijijini huku wana kilabu cha kijiji sisi miaka yote hatupati tunaomba sana kusaidiwa”alisema Ansila Kayombo

Diwani wa kata ya Ludewa Monicka Mchilo amesema lengo la kujenga kilabu cha kijiji lipo kwa kuwa fedha zipo na serikali inatambua huduma hiyo na kuwahakikishia wananchi kuwa uongozi wa kijiji unakwenda kukaa ili kuzungumza juu ya kuanza ujenzi huku mbunge wa jimbo hilo akiwaomba viongozi kuhalakisha zoezi kwa kuwa imekuwa ni kero kwa wananchi wa hali ya chini.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...