Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Uyui
KATIBU wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameupongeza Mkoa wa Tabora kwa juhudi zake za kuimarisha kilimo cha Tumbaku ambapo umeendelea kuomgeza mavuno ma mapato kwa wananchi na mkoa kwa ujumla huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa mkoa huo kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri wa kutoa mbolea ya ruzuku kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza.
Shaka amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ufumula wilayani Uyui mkoani Tabora ambapo amesema Tabora wamewekeza nguvu nyingi katika kilimo cha tumbaku, kuna mikoa 12 ambayo inalima tumbaku nchini na tuna wilaya 28 nchini ambazo zinalima tumbaku.Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 zililimwa karibia kilo milioni 37 za tumbaku nchini lakini mwaka wa fedha 2021/2022 zililimwa kilo milioni 140 nchi nzima.
“Mkoa wa Tabora mmeongoza kutoka kilo milioni 16 mpaka kilo milioni 33. Mkoa wa Tabora uliongoza na mmefanya vizuri katika kilimo cha tumbaku nataka niwaahidi kwa namna ambavyo mmefanya vizuri.Hapa Tabora mnachangamoto , naambiwa bei ya mbolea ya ruzuku inauzwa dola 70, sio sahihi. Rais Samia amewapunguzia makali wakulima wa tumbaku kutoka bei ya Sh.170,000 mpaka Sh.70,00 na yote hiyo inakwenda ndivyo sivyo kwasababu hakuna usimamizi unaoeleweka.Ndio hayo mliyoyasema tatizo linaanzia kwa Mrajisi , sijui kwa nini hakuna usimamizi unaoleweka
“Viongozi mkoa wa Tabora mnaohusika wote nendeni kasimamieni bei elekezi ya Serikali ,Rais Samia ameamua kuwapunguza ukali wa maisha wakulima wa tumbaku ,amepunguza ruzuku kwenye zao la tumbaku ama kwenye kilimo cha tumbaku
“Sio kwa bahati mbaya kwasababu anaumwa na nguvu za wananchi kusudi uzalishaji uweze kukua , pato la mwananchi mmoja mmoja liweze kukua, na pato la taifa liweze kukua kupitia kilimo cha tumbaku.Kuna mtu namsikiliza mtu mmoja hapa alikuwa akilalamika juu ya madeni akisema yapo madeni ya tumbaku yanadaiwa mpaka na hayajalipwa.
“Kwasababu mmezalisha kilo zaidi ya milioni 33 mkoa huu wa Tabora peke yake mlitengeza zaidi ya Sh.bilioni 125 katika kilimo hiki cha tumbaku msimu wa mwaka 2021/2022.Pendekezo langu kwa Serikali na kwa bahati wamepatikana wadau wengine fedha hizi zilipwe haraka,”alisema Shaka.
Ameongeza utaratibu unasema mara baada ya kuuza tumbaku malipo yafanyike ndani ya siku 14 mpaka 18 , sasa hayo madeni ameiagiza Wizara ya Kilimo kuratibu madeni hayo kuhakikisha madeni yanalipwa kabla ya msimu mpya wa kilimo haujaanza.
“Lazima kuwe na usimamizi mzuri kwenye uuzwaji wa mbolea ya ruzuku wajanja wajanja hawa mhesimiwa mkuu wa wilaya wadhibitini ambao wanataka kuhujumu jitihada za rais samia katika kuwapunguzia ukali wa maisha wakulima wa tumbaku ili tuachieni, Serikali iko hapa na ili inalibeba Serikali na litaratibiwa vizuri sana,”ameeleza Shaka.
Home
KILIMO
CCM YASHITUKIA UJANJA UJANJA UTOAJI MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA, YATOA MAELEKEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...