MSANII wa filamu za kibongo, Jimmy Mafufu ambaye pia msemaji wa wasanii amewataka wasanii kukumbuka jamii kwa kufanya maendeleo ikiwemo kurudisha kidogo wanachopata.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akitangaza rasmi harambee ya kuchqngisha fedha kwa ajili ya kukarabati shule ya msingi Sinde iliyopo Mkoani Mbeya.
Amesema asilimia kubwa ya wasanii walipotoka hasa vijijini huwa hawapeleki mchango wa aina yoyote ile.
"Mara nyingi wasanii wanajisahau walipotoka na kupelekea vijiji vyao kutopata maendelea kwa asilimia chachu ya mafanikio waliyoyapata."
Hata hivyo Mafufu ameeleza nia yake kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa Shule ya Msingi Sinde kutokana na vifo vya watoto wawili vilivotokea na kupelekea kuguswa kukarabati mazingira ya shule hiyo.
"Nimeguswa sana baada ya kusikia watoto wawili walifariki kutokna na ukuta wa shule hivyo fedha nilizozipata katika kazi yangu ya sanaa nitahakikisha natengeneza ukuta."
Msanii huyo ametoa ushauri kwa wasanii kujisajili katika chama cha wasanii ili kutambulikaa na kupewa msaada wa haraka pale wanapopata tatizo.
Hata hivyo amepongeza Kampuni ya ulinzi ya K4security kwa kuwashika mkono wasanii na kuona ipo haja ya wao kuunganao kwa ajili ya kukarabati mazingira ya shule hiyo na kuwahakikishia usalama watakapo wasili Jijini Mbeya .
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ulinzi ya K4security Biko Scanda amesema watashirikiana na wasanii hao kukamilisha ukarabati huo.
Aidha , Scanda ameeleza zaidi nia ya Kampuni hiyo katika kuwashika mkono wasanii na kueleza kuwa wanatarajia kuwanyanyua wasanii kutengeneza filamu zenye uhalisi hasa upande wa vifaa na magazine Hamish kwenye matukio.
"Wasanii wanachangamoto kubwa hususani upande wa mavazi na silaha zener uhalisia hivyo Kampuni yet imelitazama hilo kwa kina na tumehaidi kuwashika mkono kwenye hilo."Msanii wa filamu nchini Jimmy Mafufu akizungumza na Wanahabari mara baada ya kutangaza nia yake ya kufanya harambe kuchangisha fedha kwa ajili ya kukarabati mazingira ya shule ya msingi Sinde iliyopo Mkoani Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...