Kamati  ya fedha na Utawala  halmashauri  ya Mji Masasi Mkoani Mtwara  imetoa agizo kwa wataalam wote ambao wanahusika kusimamia Miradi ya maendeleo kuhakikisha wanasimamia majukumu yao mpaka pale Mradi unapokamilika.

Ameyasema hayo  0ktoba 20,2022 Mwenyeketi wa kamati ya fedha na Utawala Mh: Hashim Namtumba  ambae pia ni diwani wa kata ya Jida katika ziara ya ukaguzi  wa miradi ya Maendeleo  katika robo ya kwanza kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.

Katika ziara hiyo kamati imetembelea na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa sekondari mpya ya Temeke ,ujenzi wa Jengo la kujifungulia zahanati ya Chisegu,Ujenzi wa OPD na Maabara kituo cha Afya Mtandi ,Ujenzi wa choo Soko la Jida ,Ujenzi wa Vyumba vinne vya  Madarasa Shule ya Sekondari Anna Abdalla ,Ujenzi wa Zahanati ya Machombe .
Mwenyekiti wa kamati ya fedha na Utawala Mh: Hashim Namtumba  pamoja wataalamu wa halmashauri ya Mji Masasi wakipokea maelekezo ya ujenzi wa vyumba vya  madarasa katika shule Mpya  ya sekondari Temeke kutoka kwa Fundi Ndugu Fidelis Mpili.

Kupitia ziara hiyo kamati ya fedha ilipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Mji Masasi Elias Ntiruhungwa kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Temeke amesema kuwa Halmashauri ilipokea fedha Shilingi 470,000,000.00 ambayo   haikutosha kutekeleza Mradi Wote kulingana na Mchoro wa BOQ ya Mradi hivyo hadi kukamilisha Ujenzi  wa Majengo yote yaliyoopo kwenye  Mchoro ilihitajika fedha Shilingi 700,000,000.00.

’’Baada ya kuona fedha hazitoshi Halmashauri iliamua kuanza ujenzi  kwa kujenga Majengo ambayo yataweza kupokea wanafunzi na kufanikiwa kujenga jingo la utawala,Vumba 8 vya Madarasa ,Maabara ya kemia na biolojia ,vyoo vya wavulana na Wasichana ambavyo vimekamilika ,na Jengo la Maktaba ambalo bado halijakamilika na tunatarajia kupokea wanafunzi ifikapo januari 2023 kwa sababu shule hii tayar imeshasajiliwa’’Elias Ntiruhungwa.
Muonekano wa madarasa ya shule Mpya ya Sekondari Temeke
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi Elias Ntiruhungwa akitoa Maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Temeke ambao umegharimu fedha Shilingi 470.000.000.00.

Baada ya kupokea maelezo hayo kamati imepongeza menejimenti  kwa mawazo mazuri ambayo pamoja na Majango kutokamilika kulingana na Mchoro  kama  ulivokuwa unatakiwa  ukamilishwe ila ni hatua ambayo imeleta matumaini yakuweza kutumika  pale ifikapo January 2023.

Katika ziara hiyo kamati ya Fedha na Utawala imekagua ujenzo wa jengo la kujifungulia Zahanati ya Chisengu  ambapo Mtendaji  Kata Zakia Maguno  alisoma Taarifa ya Mradi na kueleza  vyanzo  vya  fedha  vya Mradi huo kuwa ni Mfuko wa Jimbo  ulitoa Shilingi 14,100,000 Nguvu za wananchi   Shilingi  500,000  Mfuko wa Afya Shilingi 3,795,000 pamoja na mapato ya Ndani ya halmashauri   Shilingi 1,000,000 na Jumla kuu  ni Shilingi 19,395,000  ambayo imeweza kukamilisha Mradi huo.

Kamati imepokea taarifa hiyo na kuridhia kwani Maendeleo ya Mradi ni  Mazuri yanaonekana na Thamani ya fedha iliyotumika ni sahihi pia wametoa Shukrani kwa halmashauri ya Mji Masasi kwa kuwawezesha kukamilika kwa Mradi huo ambao ni msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo.

Vilevile kamati ilifanya ziara katika ujenzi wa zahanati ya Machombe ambapo wajumbe walishuhudia juhudi zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo ambapo Mradi  huo utagharimu kiasi cha fedha  shilingi  106,776,692.00 mpaka kukamilika na hadi sasa Meadi umepokea Fedha shilingi  62,000,000 ikiwa mradi upo hatua  ya  uchapiaji.

Hivyo kamati imeridhishwa na mradi huo baada ya kukaguwa na wametoa pongezi kwa wasimamiz wa Mradi huo pia kamati imeshauri zifuatwe taratibu zote za manunuzi ili kuepuka hoja za kiukaguzi pia wametoa agizo kwa Mhandisi wa halmashauri ya Mji Ombeni Usiri kuandaa BOQ kwa ajili ya ujenzi wa choo ambayo itatumika baada ya kunza kutoa huduma katika zahanati hiyo.
Muonekano wa ujenzi wa jengo la Zahanati ya Machombe kata Marika Halmashauri ya Mji Masasi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...