Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakifuatilia taarifa ya utendaji wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), iliyowasilishwa kwao na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, jijini Dodoma.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), bwana Lazaro Kilahala akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati Wakala huo ulipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi kwa mwaka 2022/23 kwa kamati hiyo jijini Dodoma.Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya utendaji ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), iliyowasilishwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...