Na Mwandishi wetu, Mirerani
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Kiria Laizer ameongoza
harambee ndogo ya kumchangia mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa chuo
cha utumishi wa umma Tanga anayesomea diploma ya utunzaji kumbukumbu ya
nyaraka.
Kiria, ameongoza
shughuli ya kumchangia msichana huyo Maureen Laizer ambaye anaishi na
mama yake kwenye kata ya Endiamtu na kufanikisha kupata shilingi
500,000.
Awali, harambee
hiyo ngodo ilifanyika na kupatikana shilingi 200,000 ila Kiria
akaongezea shilingi 300,000 na kupatikana shilingi 500,000
zitakazotumika kwenye masomo ya mwanafunzi huyo.
Kiria
akizungumza kwenye shughuli hiyo ya harambee amesema kuchangia elimu ni
jambo jema kwenye jamii kwani hivi sasa msingi mzuri wa watoto ni
kupatiwa elimu.
“Mtoto
huyu amejitahidi hadi kufikia hatua hii ya kuwa mwanafunzi wa chuo hivyo
ni vyema akasaidiwa ili aweze kuhitimu masomo yake anayosomea mkoani
Tanga,” amesema Kiria.
Mwenyekiti
wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Adam Kobelo amewapongeza viongozi
na wananchi waliochanga na pia Kiria kwa kufanikisha harambee hiyo ndogo
kwa kutoa fedha zake binafsi shilingi 300,000.
Hata
hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera amemtaka
mwanafunzi huyo kuhakikisha anasoma kwa bidii ili aweze kutimiza ndoto
zake na pia kutumikia Taifa hapo baadaye.
“Pia
unapaswa kutambua kuwa hakuna haki isiyokuwa na wajibu, unachangiwa
fedha za masomo lakini ofisa mtendaji wa kata atafuatilia huko chuoni
kwenu ili kuangalia maendeleo yako,” amesema Dk Serera.
Kwa
upande wake mwanafunzi huyo Maureen amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya,
Mwenyekiti wa CCM na viongozi wote waliofanikisha yeye kuchangiwa na
kupata fedha hizo za ada za masomo.
“Nawashukuru
wote waliofanikisha mimi kupata msaada huu wa ada ya masomo na
ninawaahidi kusoma kwa bidii kwenye masomo yangu huko chuoni Tanga,”
amesema.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Kiria Laizer (kushoto)
akimkabidhi shilingi 5,000 mwanafunzi wa stashahada ya utunzaji
kumbukumbu ya nyaraka katika chuo cha utumishi wa umma Tanga, Maureen
Laizer kwa ajili ya ada ya masomo yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...