MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema ni muhimu kwa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kuangalia pengo la Kisera katika mfumo wa ukusanyaji mapato nchini na kuufanyia mageuzi sahihi ili kuongeza ufanisi na kukuza kiwango cha mapato Zanzibar.

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipozungumza na Kamshina wa ZRB ndugu Ramadhani Juma Mwenda aliyefika ofisini kwa Makamu kujitambulisha na kubadilishana naye mawazo kuhusu masuala mbali mbali yanaoweza kuchangia ufanisi na kukuza kiwango cha mapato yanayokusanywa Zanzibar.

Mhe. Makamu amefahamisha kwamba yapo maeneo mengi ya Mapato ambayo yanaweza kufanyiwa mageuzi zaidi ya kisera na kisheria jambo litakalochangia kuongeza kiwango cha mapato yanayokusanywa kupitia vyanzo tofauti vilivyopo nchini.

Aidha Mhe. Othman amesema hatua ya hiyo pia itasaidia sana kuwepo vyanzo zaidi vya mapato yatakayoweza kuchangia kasi zaidi ya maendeleo ya nchi kutokana na kiwango kikubwa zaidi cha mapato kuweza kukusanywa.

Mhe. Othman amesema kwamba yapo maeneo mengi ambayo baada ya mageuzi ya kisera na kisheria kufanyika yataweza kutumika kukusanyia mapato zaidi na nchi ikaweza kuendelea kwa kasi kubwa kwa kiwangpo cha mapato yatakayopatikana kuliko ilivyo sasa.

Pia Mhe. Othman amesema kwamba kuna haja ya kuchambua zaidi viwango vya malipo vinavyokana na ushuru wa stamp hasa katika kutafautisha mapato ya aina hiyo kupitia miradi mikubwa na inayoanzishwa nchini ile ya kawaida ambapo viwango vyake vinaweza kuwa tafuati kuliko ilivyo sasa.

Aidha amesema kwamba kuna fursa nyingi za mikopo ya kifedha katika mabenki mbali mbali nchini zinazoweza kutumika kibiashara lakini zimekuwa zikitumika zaidi kwa bikopo ya watu binafsi kuliko mashirika ambayo yanaweza kuwa na kiwango cha tija zaidi katika kasi ya ukusanyaji mapato nchini.

Amefahamisha kwamba pia eneo la utayarishaji wa mikataba ya kibisashara kupitia watu binafsi, mashirika na taasisi nalo ni muhimu kuangaliwa kwani linaweza kusaidia kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato na kuchangia kasi zaidi ya kukuza uchumi wa Zanzibar.

Mhe. Othman ameshauri pia katika jitihada za kuongeza kiwango cha mapato bodi hiyo kuangalia uwezekano katika utaratibu wa Benki za Kiisalamu kwa kuwa bado kunachangamoto kwenye eneo hiilo na itakapotatuliwa itachangia kiwango cha mapato kuongezeka nchini.

Naye Kamshida wa Bodi hiyo ndugu Ramadhani Juma Mwenda, ameeleza kwamba ZRB inaendelea kufanya mageuzi katika mifumo yake ya ndani ya ukusanyaji mapato jambo linalochangia kuongeza kiwango cha mapato yanayokusanywa Zanzibar kupitia bodi hiyo.

Amesema kwamba kutokana na hali hiyo wamefanikiwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 131 hadi 135 kwa kipindi cha miezi mitatu.

Amesema pia jitihada kubwa imefanywa katika kudhibiti udanganyifu na uvujaji wa mapato sambamba na kutengeneza mazingira bora ya ulipatiji kodi za aina mbali mbali jambo linalochangia kuongeza ufanisi na mafanikio zaidi ya kukusanya kodi.



MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na Kamshina wa Bodi ya Mapato Zanzibar ND. Ramadhan Juma Mwenda (kulia kwa makamu), aliyefika Ofisini kwa Makamu Migombani Kujitambulisha leo tarehe 17.10.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Kitengo cha Habari.



MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , (kulia) akizungumza na Kamshina wa Bodi ya Mapato Zanzibar ND. Ramadhan Juma Mwenda , aliyefika Ofisini kwa Makamu Migombani Kujitambulisha leo tarehe 17.10.2022. kulia kwa Kamshina ni Ofisa Uhusiano wa ZRB ndugu Makamue Khamis Mohammed. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Kitengo cha Habari.



MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akisalimiana na na Kamshina wa Bodi ya Mapato Zanzibar ND. Ramadhan Juma Mwenda (kushoto kwa makamu), aliyefika Ofisini kwa Makamu Migombani Kujitambulisha leo tarehe 17.10.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Kitengo cha Habari


MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na Kamshina wa Bodi ya Mapato Zanzibar ND. Ramadhan Juma Mwenda (kulia kwa makamu), aliyefika Ofisini kwa Makamu Migombani Kujitambulisha leo tarehe 17.10.2022. kulia kwa Kamshina na Ofisa wa Kitengo cha Uhusiano ZRB ndugu Makame Khamis Mohammed. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Kitengo cha Habari.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na Kamshina wa Bodi ya Mapato Zanzibar ND. Ramadhan Juma Mwenda (kulia kwa makamu), aliyefika Ofisini kwa Makamu Migombani Kujitambulisha leo tarehe 17.10.2022. kulia kwa Kamshina na Ofisa wa Kitengo cha Uhusiano ZRB ndugu Makame Khamis Mohammed. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Kitengo cha Habari


MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia) , akiwa katika picha ya pamoja na Kamshina wa Bodi ya Mapato Zanzibar ND. Ramadhan Juma Mwenda , aliyefika Ofisini kwa Makamu Migombani Kujitambulisha leo tarehe 17.10.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza Kitengo cha Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...