RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, wakati alipotembelea banda la Mfuko kabla ya kufungua Maonesho ya 3 ya Viwanda na Biashara Mkoa wa Pwani. NSSF inashiriki Maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kueleza fursa mbalimbali za Uwekezaji, kutatua kero za wanachama na kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Maonesho hayo yanaendelea katika stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani na yatafikia kilele tarehe 10/10/2022
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...