Na Mwandishi Wetu, Same
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo amefungua Kongomano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere ambalo pamoja na mambo mengine limejadili maono mbalimbali ambayo baba wa taifa aliyoyafanya henzi za uhai wake.
Mpogoro wakati akifungua kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina jitihada ambazo zilifanywa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja na kudumisha mshikamano huku akipenda kuona watu wake wanapiga hatua kimaendeleo.Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki,Jacob Koda ameiomba Serikali kufufua Viwanda vyote vilivyokuwa vikifanya uzalishaji enzi za Mwalimu Nyerere ikiwa kama njia mojawapo ya kumuenzi Mwalimu.
Kwa upande wake Askofu Koda aliyasema hayo wakati akitoa mada kuhusu Mchango wa Mwalimu katika kukuza uchumi na Maendeleo endelevu ambapo alisema Nyerere alijitahidi kuanzisha viwanda katika mikoa mbalimbali ili kukuza uchumi.
Alisema Baba wa Taifa alitambua ili nchi iweze kuwa na Maendeleo endelevu lazima kuwe na viwanda na ndipo alipoanzisha viwanda vya nguo kwenye mikoa karibu yote,kulikuwepo na viwanda vya ngozi vikitengeneza viatu,mabegi,kulikuwepo na viwanda vya magunia na kiwanda Cha General Tyre cha Arusha ambacho kilikuwa kinaaaminika kwa matairi bora Afrika Mashariki.
Wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyekuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo aliahidi kuuchukua ushauri huo wa Askofu na kuufanyia kazi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...