Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kutoa taarifa juu ya
taratibu za kupata vibali vya uratibu wa Maonesho (Trade Fairs and Exhibitions),
Makongamano, Misafara ya Kibiashara (Trade Missions) pamoja na shughuli nyingine za
Ukuzaji Biashara (Trade Promotional Events) ndani na nje ya Nchi.

Kifungu cha 5(1) (b) cha Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade), Na. 4 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake, kimeipa TanTrade
mamlaka ya kuunganisha na kudhibiti Soko la Ndani (Integrate and Regulate Domestic
Market). Uratibu wa shughuli za Ukuzaji Biashara ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa
hayo. Kadhalika, Kifungu cha 5(1), (p) cha Sheria hiyo pamoja na Aya ya 3(1)(k) ya Kanuni
za Sheria ya TanTrade za mwaka 2010, vinaipa TanTrade mamlaka ya kumruhusu/ kutoa
kibali kwa mtu yeyote, Taasisi au Shirika lolote kuandaa Maonesho ya ndani (local) na ya
Kimataifa (International).

TanTrade imepokea malalamiko ya baadhi ya washiriki wa Misafara ya Kibiashara ambayo
imefanyika bila waandaaji wa misafara hiyo kupata Kibali cha TanTrade. Baadhi ya
Waandaaji wa misafara hiyo, hawatimizi ahadi na mahitaji kwa wateja/washiriki kama
yalivyoainishwa kwenye matangazo ya misafara hiyo na kulingana na gharama zilizolipwa
na washiriki. Kadhalika, baadhi ya waandaaji wa shughuli za ukuzaji biashara kama
Maonesho na misafara ya Kibiashara wamekuwa wakitumia picha za baadhi ya Viongozi
wa Serikali katika matangazo ya shughuli hizo bila ya kibali ama ridhaa ya Viongozi husika.
Waandaaji hao wamekuwa wakiupotosha Umma kupitia mitandao ya kijamii kama vile
Instagram, Whatsapp na facebook kwamba TanTrade inawaonea na kuwanyima vibali vya
kuandaa shughuli za ukuzaji Biashara, jambo ambalo sio la kweli. TanTrade inapenda
kusisitiza kuwa itaendelea kutoa vibali kwa watu binafsi, Kampuni, Taasisi na Asasi
ambazo zimekidhi vigezo vya kuratibu shughuli za ukuzaji wa biashara bila kumwonea mtu
yeyote. Tunatoa wito kwa waandaaji wote wa shughuli za Ukuzaji Biashara kufuata Sheria
na Taratibu zilizopo ili kuondoa usumbufu na utapeli katika Sekta hii kwa maslahi ya Taifa
letu.
Kadhalika, tunatoa angalizo kwa Umma kuwa, ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kabla
ya kushiriki shughuli yoyote ya ukuzaji Biashara iliyoandaliwa na Kampuni au Taasisi
yoyote, ni vema kupata uthibitisho ikiwa mwandaaji amepata idhini ya TanTrade ya
kuandaa shughuli husika.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia namba 0733 002 014 au tembelea tovuti
yetu www.tantrade.go.tz au fika katika Ofisi zetu zilizopo katika Uwanja wa Maonesho wa
Mwl. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam au Jengo la Kilimo V, Barabara ya VETA
nyuma ya CBE, Dodoma na Zanzibar, Kijangwani, Jengo la Posta.
Imetolewa na:
Daniel J. Diah
Afisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...